031-Luqmaan: Utangulizi Wa Suwrah

 

031-Luqmaan: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.

 

Idadi Za Aayah: 34

 

Jina La Suwrah: Luqmaan

 

Suwrah imeitwa Luqmaan, na inayodalilisha ni kutajwa mja mwema huyo katika Aayah namba (12-13).

 

Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:

 

1-Amri juu ya kufata hikma iliyokuja kwenye Qur-aan, na tahadhari kwa atakaeipuuza. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]

 

2-Kuthibitisha na kuisifu Qur-aan Tukufu katika sifa mbali mbali ikiwemo sifa ya hikma, na ambayo inahitaji hikma ya Aliyeiteremsha (سبحانه وتعالى), katika Maneno na Matendo Yake. Na kisa cha Luqmaan aliyejaaliwa hikma na Allaah (سبحانه وتعالى), ambaye ndio jina la Suwrah hii, ni mojawapo ya ushahidi wa wazi wa hili.

 

3-Kuwasifia Waumini kwa sifa mbalimbali.  

 

4-Kuisemesha nafsi ya mwanaadam kwa mambo yatayoifanya iishi vizuri na maisha ya raha.

 

Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:

 

1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama  الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imtukuzwa Qur-aan kuwa ni ya hikma, na kwamba Qur-aan ni mwongozo kwa watu, na ni rehma kwa Waumini, Wahisani pamoja na kutajwa sifa zao.

 

2-Ikataja baadhi ya sifa ya washirikina, ambao wanazifanyia mchezo Aayah za Allaah.

 

3-Imetaja dalili za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Uumbaji Wake na Uwezo Wake wa kuumba mbingu bila ya kuwa na nguzo, na kuumba ardhi na vilivyomo humo pamoja na Neema Zake humo kwa watu.

 

4-Imetajwa kisa cha Luqmaan na hikma alizojaaliwa nazo; miongoni mwazo ni wasia wake kwa mwanawe uliokusanya daawah ya Tawhiyd na kusimamisha Swalaah, na tabia njema, na kutokuwa na kiburi.

 

5-Imetajwa kuwa kuna Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) zenye kuonekana na zisizoenekana.  

 

6-Imetajwa kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya kutowaamini washirikina.

 

7-Imetajwa zingatio kubwa la kuwa Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni mengi mno hayawezi kuhesabika wala kumalizika wala hayana mwisho!

 

8-Imewalingia watu wote kuwa na taqwa ya Allaah, na kutodanganyika na dunia.

 

9-Suwrah imekhitimishwa kwa kutaja mambo matano ya ghaibu ambayo hakuna ayajuae isipokuwa Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى).

  

 

 

 

Share