11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Anaweza Kumsemesha Mwanaume Kama Fitnah Haipo Na Kwa Vidhibiti Vya Kisheria

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

 

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

 

11-Mwanamke Anaweza Kumsemesha Mwanaume Kama Fitnah Haipo Na Kwa Vidhibiti Vya Kisheria:

 

Kumsemesha huku kunatakikana kuwe kunatokana na dharura na haja pamoja na kuwajibika na vidhibiti vya kisharia.  Asilegeze maneno, akayalainisha, akayalaza.  Na hii ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:

 

فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

 

“Basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi, na semeni kauli inayokubalika”.  [Al-Ahzaab: 32].

 

Na jingine linalodulisha kuruhusika hilo ni Neno Lake Ta’aalaa:

 

"وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ"

 

Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia”.  [Al-Ahzaab: 53].

 

Na Neno Lake Ta’aalaa kuhusu Nabiy Muwsaa ‘alayhis Salaam kuwasemesha wanawake wawili wa Madyana:

 

"وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ  • فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا"

 

“Na akakuta kando yake wanawake wawili wanawazuia (wanyama wao). Akasema:  Mna nini?  Wakasema:  Hatunyweshi mpaka waondoke wachungaji, na baba yetu ni mtu mzima sana  •  Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema:  Rabb wangu!  Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia  •  Basi akamjia mmoja kati ya wanawake wawili akitembea kwa kuona hayaa, akasema:  Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea”.  [Al-Qaswas: 23-25]

 

Maudhui hii ina Hadiyth nyingi tu.  Kati yake ni ya Anas:

 

"لَمَّا ثَقُلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَعَلَ يَتَغَشَّاهُ الكَرْبُ، فَقَالَتْ فَاطِمَةُ عَلَيْهَا السَّلاَمُ: وَاكَرْبَ أَبَاهُ‏.‏ فَقَالَ لَهَا: "‏لَيْسَ عَلَى أَبِيكِ كَرْبٌ بَعْدَ الْيَوْمِ ‏"‏‏.‏‏ فَلَمَّا دُفِنَ قَالَتْ فَاطِمَةُ عَلَيْهَا السَّلاَمُ : يَا أَنَسُ، أَطَابَتْ أَنْفُسُكُمْ أَنْ تَحْثُوا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ التُّرَابَ"

 

“Maradhi yalipomzidia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ghamu kubwa ilianza kumtamalaki.  Faatwimah (‘alayhas Salaam) akasema:   Dhiki na tabu iliyoje kwa baba yangu!  Akamwambia:  Ghamu na dhiki hatoipata tena baba yako baada ya leo.  Alipozikwa, Faatwimah (‘alayhas Salaam) alimwambia Anas:  Ee Anas!  Je mlijisikia vizuri kummiminia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mchanga!”.  [Swahiyhul Bukhaariy (4462)].

 

 

 

Share