11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

11-Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu:

 

Ya kwanza:  Baada ya kuhirimia Hajji au ‘Umrah:

 

Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na aliyehirimia Hajji au ‘Umrah:

 

"وَلاَ تَلْبَسُوا مِنَ الثِّيَابِ شَيْئًا مَسَّهُ الزَّعْفَرَانُ وَلاَ الْوَرْسُ"

 

 “Wala msivae nguo yoyote iliyoingiwa na zafarani wala wars”….  [Al-Bukhaariy.  Takhriyj yake iko kwenye mlango wa Hijja]

 

Hikma ya kuzuiwa mwanamke aliyehirimia, ni kuwa harufu ya mafuta haya ni katika vichangamshi na vichochezi vya jimai ambayo inaharibu ihraam.

 

Ya pili:  Katika eda

 

Mwanamke anakatazwa kutumia mafuta mazuri wakati wa eda ya kufiwa na mumewe.

 

Ya tatu:  Anapotoka nyumbani

 

Na hii ni hata kama atamkusudia mumewe kama tulivyotangulia kugusia hili nyuma kidogo.

 

 

Share