022-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ipi Dalili Ya Sharti La Kufuata, Kwa Mujibu Wa Qur-aan Na Sunnah?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

022-Ipi Dalili Ya Sharti La Kufuata, Kwa Mujibu Wa Qur-aan Na Sunnah?

 

 

Swali:

 

س: ما دليل اشتراط الانقياد من الكتاب والسنة 

 

Ni ipi dalili ya sharti la kufuata, kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah?

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى ( ومن يسلم وجهه إلى الله وهو محسن فقد استمسك بالعروة الوثقى ) وقال النبي صلى الله عليه وسلم ( لا يؤمن أحدكم حتى يكون هواه تبعا لما جئت به ).

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) Anayosema:

 

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾

 

Na anayesilimisha uso wake kwa Allaah, naye ni mtenda wema, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. Na kwa Allaah ni mwisho wa mambo yote. [Luqmaan (31:22)]

 

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema:

 

  ((لاَيُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَواهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ))

Haamini mmoja mwenu mpaka hawaa (matamanio) yake yawe ni kufuata nilichokuja nacho. [Imepokewa na Ibn Abi ‘Asim katika kitabu Sunnah, Al-Baghwi katika Sharhi Sunnah, Al-Khatwib katika At-Taarikh (4/369), Ibn Batwa katika Al-Inabah kitabul Imaan na sanad yake imepita kwa Naim bin Hammad ambaye ni dhaifu, kama ilivyo pokewa kutoka kwa ibn ‘Amru ambaye ni Jahala (hafahamiki), Hadiyth hii ipo katika 40 Nawawi na amesema kuwa ni sahihi. Ibn Rajab alishindana nae kwa kusema: usahihi wake uko mbali kwa kuwa Naim ameipokea peke yake, wametofautiana katika sanad yake kama vile katika sanad yupo ‘Uqbah bin ‘Awf ambaye hafahamiki vile vile].

 

 

Share