029-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Kushuhudia Ya Kuwa Muhammad Ni Rasuli Wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

029-Nini Maana Ya Kushuhudia Ya Kuwa Muhammad Ni Rasuli Wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

Swali:

 

س: ما معنى شهادة أن محمدا رسول الله صلى الله عليه وسلم 

 

Nini maana ya Kushuhudia ya kuwa Muhammad ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

Jibu:

 

ج: هو التصديق الجازم من صميم القلب المواطئ لقول اللسان بأن محمدا عبده ورسوله إلى كافة الناس إنسهم وجنهم( شاهدا ومبشرا ونذيرا وداعيا إلى الله بإذنه وسراجا منيرا )فيجب تصديقه في جميع ما أخبر به من أنباء ما قد سبق وأخبار ما سيأتي وفيما أحل من حلال وحرم من حرام والامتثال والانقياد لما أمر به والكف والانتهاء عما نهى عنه واتباع شريعته والتزام سنته في السر والجهر مع الرضا بما قضاه والتسليم له وأن طاعته هي طاعة الله ومعصيته معصية الله ;لأنه مبلغ عن الله رسالته ولم يتوفه الله حتى كمل به الدين وبلغ البلاغ المبين وترك أمته على المحجة البيضاء ليلها كنهارها لا يزيغ عنها بعده إلا هالك وفي هذا الباب مسائل ستأتي إن شاء الله.

 

Ni kukubali moja kwa moja ndani ya moyo, sambamba na kutamka kwa ulimi kwamba Muhammad ni mja na Rasuli Wake kwa watu wote bin-Aadam na majini

 

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji.

وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾

Na mlinganiaji kwa Allaah kwa Idhini Yake, na siraji kali yenye nuru. [Al-Ahzaab: (33:45-46)]

 

Kwa hiyo  inapasa kumsadikisha katika yote aliyoyaeleza, habari zilizopita na habari zijazo, katika aliyohalalisha, na aliyoharamisha kufuata na kunyenyekea aliyoyaamrisha, kujizuia na kukoma kwa aliyoyakataza, kufuata shariy’ah yake na kulazimu Sunnah yake katika siri na jahara pamoja na kuridhia hukumu yake na kujisalimisha kwake, na kuwa kumtii yeye ni kumtii Allaah, kwa kuwa yeye ni mfikishaji wa Allaah na kumuasi yeye ni kumuasi Allaah, na kuwa Allaah hakumfikisha hadi alipokamilisha dini  na akafikisha kufikisha kwa bayana akaacha uma wake kwenye uwanja mweupe usiku wake ni kama mchana wake hapotei (njia) hiyo baada yake, isipokuwa upotevu, katika mlango huu kuna maswali yatakuja In shaa Allaah.

 

 

Share