047-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Hiyo Shirki Ndogo?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

047-Ni Ipi Hiyo Shirki Ndogo?

 

 

Swali:

س: ما هو الشرك الأصغر

Ni Ipi hiyo shirki ndogo?

 

Jibu:

 

ج: هو يسير الرياء الداخل في تحسين العمل المراد به الله تعالى قال الله تعالى ( فمن كان يرجو لقاء ربه فليعمل عملا صالحا ولا يشرك بعبادة ربه أحدا )وقال النبي صلى الله عليه وسلم( أخوف ما أخاف عليكم الشرك الأصغر )فسئل عنه فقال( الرياء )ثم فسره بقوله صلى الله عليه وسلم( يقوم الرجل فيصلي فيزين صلاته لما يرى من نظر رجل إليه ) ومن ذلك الحلف بغير الله كالحلف بالآباء والأنداد والكعبة والأمانة وغيرها قال صلى الله عليه وسلم( لا تحلفوا بآبائكم ولا بأمهاتكم ولا بالأنداد )وقال صلى الله عليه وسلم( لا تقولوا والكعبة ولكن قولوا ورب الكعبة )وقال صلى الله عليه وسلم( لا تحلفوا إلا بالله) وقال صلى الله عليه وسلم( من حلف بالأمانة فليس منا )وقال صلى الله عليه وسلم( من حلف بغير الله فقد كفر أو أشرك )وفي رواية( وأشرك )ومنه قول ما شاء الله وشئت قال النبي صلى الله عليه وسلم للذي قال له ذلك ( أجعلتني لله ندا بل ما شاء والله وحده )ومنه قول لولا الله وأنت وما لي إلا الله وأنت وأنا داخل على الله وعليك ونحو ذلك, قال صلى الله عليه وسلم( لا تقولوا ما شاء الله وشاء فلان ولكن قولوا ما شاء الله ثم شاء فلان )قال أهل العلم ويجوز لولا الله ثم فلان ,ولا يجوز لولا الله وفلان.

 

Ni kufanya jambo jema kwa niyyah ya kujionyesha. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

 فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾

Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende amali njema na wala asimshirikishe yeyote katika ibaada za Rabb wake. [Al-Kahf: (18:110)]

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Kitu ninachokihofia zaidi kwenu ni shirki ndogo”.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaulizwa kuhusiana na Shirki hiyo na Nabiy akasema:

 

"Ni kujionyesha".

 

Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaelezea shirki hiyo kwa kusema:

 

"Ni mtu kuswali na kuirembesha Swalaah hiyo baada ya kuona jicho la mtu likimwangalia yeye”.

 

Na miongoni mwa shirki ndogo ni mtu kuapa kwa asiyekuwa Allaah kama vile kuapa kwa baba zake, au wapenzi wake, au Al-Ka'abah na Amana na vinginevyo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Msiape viapo kwa baba zenu, wala kwa mama zenu, au kwa vipenzi vyenu".

 

Na Nabiy (Swalla Allaau 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Msiseme na Al-Ka'abah, ila semeni na Rabb wa Al-Kaabah".

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

 

"Msiape isipokuwa kwa Allaah".

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

“Mwenye kuapa kwa dhamana sio katika sisi”.

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah, hakika amekufuru au amemshirikisha Allaah”.

 

Na katika riwaayah nyingine:

 

“Na akamshirikisha”.

 

Na katika kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: lile Analotaka Allaah na wewe Nabiy.

 

Kauli hii alimwambia yule ambae amesema kwa kiapo hicho kwa kumwambia:

“Je umenifanya mimi ni mshirika wa Allaah? Bali sema Akitaka Allaah Pekee.”

 

Na kauli nyingine ni: Lau sio Allaah na wewe, Nina nini mimi na Allaah, na mimi nipo katika miliki ya Allaah na wewe na wengineo,  na mfano wa hayo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema:

 

"Msiape kwa kusema Akitaka Allaah na fulani, lakini semeni: Akitaka Allaah, kisha fulani”.

 

Wanachuoni wamesema: Inafaa kusema Akitaka Allaah kisha fulani, na sio kusema Akitaka Allaah na fulani.

 

 

Share