16-Malaika: Mbawa Za Malaika

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

16:  Mbawa Za Malaika

 

Allaah Ta’aalaa Anasema:

 

"الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۚ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ"

 

AlhamduliLLahi (Himdi Anastahiki Allaah), Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mwenye Kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, tatu-tatu na nne-nne. Huzidisha katika uumbaji Atakavyo.  Hakika Allaah Ni Muweza juu ya kila kitu”.  [Faatwir: 01]

 

Ibn Kathiyr amesema:  “Kuna Malaika wenye mbawa mbili mbili, wengine tatu tatu, wengine nne nne, na wengine zaidi ya hapo.   Huzitumia kuruka haraka ili kwenda kufikisha yale waliyotumwa na Allaah kuyafikisha au kuyafanya, au kutekeleza jukumu lolote walilokalifishwa”.

 

‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona Jibriyl akiwa na mbawa mia sita”.

 

Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"إِذَا قَضَى اللَّهُ فِي السَّمَاءِ أَمْرًا ضَرَبَتِ الْمَلاَئِكَةُ بِأَجْنِحَتِهَا خُضْعَانًا لِقَوْلِهِ كَأَنَّهُ سِلْسِلَةٌ عَلَى صَفْوَانٍ فَإِذَا فُزِّعَ عَنْ قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ"

 

“Allaah Anapopitisha amri mbinguni, Malaika Hupiga mbawa zao kwa ajili ya kulitii Neno Lake ambalo ni kama sauti ya mnyororo (unaoburutwa) juu ya mwamba.  Na fazaiko linapoondoka nyoyoni mwao huuliza:  Nini Amesema Mola wenu?  (Malaika wabebao ‘Arshi) hujibu:  Ni haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa,  Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa”.  [Hadiyth Swahiyh.  Al-Bukhaariy (4800)]

 

Kwa haya, tunapata kujua kwamba kuna Malaika wenye mbawa mbili mbili, wenye tatu tatu, wenye nne nne na wenye zaidi ya hapo.  Jibriyl pekee ameelezewa kuwa anazo mia sita, na wengineo kama wabebao ‘Arshi, Miykaaiyl na Israafiyl hakuna ajuaye isipokuwa Allaah Pekee.

 

 

Share