36-Malaika: Malaika Wanazungumza

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

36:  Malaika Wanazungumza

 

Allaah Ta’alaa Amesema:

 

"وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ"

 

“Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika:  Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa.  Wakasema:  Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himidi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako?  (Allaah) Akasema:  Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua ● Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionesha mbele ya Malaika; Akasema:  Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli ● Wakasema: Utakasifu ni Wako hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza; hakika Wewe Ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote”.  [Al-Baqarah: 30-32]

 

Hapa, Malaika hawa walikuwa wanazungumza na Allaah Ta’alaa.  Malaika hawa pia wanazungumza wao kwa wao, na Allaah Pekee Ndiye Ajuaye lugha yao hiyo. Allaah Ta’aalaa Anatuambia tena:

 

"حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ"

 

Mpaka litakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao watasema (Malaika):  Amesema nini Rabb wenu?  Watasema:  Ya haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa,  Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa”.  [As-Sajdah: 23]

                                                  

 Ibn ‘Uthaymiyn amesema:  “Aayah hii inatuthibitishia kwamba Malaika wanazungumza, wanafahamu na wana akili.  Tunaona kwenye aayah hii baadhi wanauliza wengine kuhusu maneno Aliyoyasema Allaah, na wengine wanajibu kuwa Amesema haki.  Hii ni kinyume na wale wanaodai kwamba Malaika hawana sifa hiyo, na kwa madai yao hayo itakuwa na maana kwamba sisi tumepokea sharia ya dini na mengineyo kutoka kwa viumbe wasio na akili.  Na hii bila shaka ni kuitia dosari sharia, na jambo lisiloingia akilini”.

 

 

Share