Bid’ah – Vipengele Vyake, Madhara Na Ufumbuzi
Muhammad El Maawy
Vipengele vya Bid’ah:
Baadhi ya vipengele vya Bid’ah ni
1. Kila bid’ah ni Dhwalaalah.
Kilugha Bid’ah ni kitu chochote kipya au kitu ambacho hakijafanywa kabla, yaani, hakina mfano kabisa wa mbeleni. Katika muono wa kisheria, kila Bid’ah ni Dhwalaalah na hakuna Bid’ah hasanah au sayyi’ah (Bid’ah nzuri na mbaya). Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika hadith, “Kullu Bid’atin dhwalaalah wa kullu dhwalaalatin fin naar (kila Bid’ah ni Dhwalaalah na kila Dhwalaalah ni motoni)” (Imepokewa na Imam Ahmad, Abu Dawud, at-Tirmidhy na wengineo).
Dhalalah ina maana ya kwenda kombo au kufuata njia ya upotevu na kwenda kinyume na ukweli. Tukitazama Qur-aan, tutaona vipi Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) ametumia neno
2. Bid’ah inafanywa
Kwa maneno mengine, yeyote anayefanya bid’ah, anadai kwa kufanya hivyo atakuja karibu na Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala). Hii ni tofauti kabisa na kufanya dhambi
Hivyo, sehemu ya wazo hili la bid’ah ni kuwa yule mwenye kufanya hudai kwamba linakubaliwa na dini pamoja na Sheria na ni lenye kumpendeza Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala). Hii ndio nukta inayogawanya baina ya bid’ah na jambo lisilokuwa bid’ah.
3. Bid’ah inaweza kuwa kuanzisha kitendo kipya na pia kukibadilisha kitendo kilichokuwepo mwanzo.
Maana yake ni, pale mtu anapoanzisha kitendo kipya huku akidai kuwa kitendo hicho kimekubaliwa na Sheria bila dalili yeyote ni bid’ah. Kwa namna hiyo hiyo, pale mtu anapoacha kitu Fulani akidai kuwa kwa kuacha kitu hicho basi anamridhisha Allaah na hana dalili yeyote kutoka kwa Qur-aan au Sunnah, hiyo pia inakuwa bid’ah. Kwa mfano, wakati wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walikuja watu watatu katika nyumba zake na kuwauliza wakeze kuhusu Ibadah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), walipoelezewa waliona ni
4. Kila kitu katika Sheria kinaweza kuwa na bid’ah inayotengenezwa au kuhusiana nayo.
Sheria imejumlisha itikadi, ibadah na biashara au muamala na watu. Hivyo, bid’ah si mambo katika itikadi pekee au mambo ya ibadah lakini inaweza kuwa hata katika biashara na muamala. Kwa mfano, ikiwa mtu atadai ya kwamba kunahitajika mashahidi wanne katika mapatano ya kibiashara na wala sio wawili
5. Bid’ah haina dalili katika Qur-aan, Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala haikukubaliwa na Ijmaa (kongamano) ya Masahaba.
Mfano maarufu ambao unatajwa na watu wa bid’ah (Ahl-Bid’ah) katika yale matamanio
Kwa mfano Allaah katika Qur-aan Anatuelezea kuhusu Sunnah Zake. Bila shaka ni kuwa yeyote anapotaja kuhusu sunnah, inarudi kwa sunnah za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na vipengele vyake vya kisheria. Hivyo hivyo pale ‘Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) alipotaja hizi Swala za tarawehe za kila siku, alikuwa anamaanisha ile maana yake ya kilugha. Dalili ya dai hili lipo wazi kabisa. Swala ya Tarawehe haikuwa ni jambo geni katika dini. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alianzisha swalah hizi, na sababu ya pekee iliyomfanya yeye aache inaelezwa wazi katika hadithi zake ya kwamba hataki Ummah wake upate shida kwa swalah hiyo kufanywa faradhi. Hata hivyo, alipofariki Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), risala ya Uislamu ilikuwa imekamilishwa na swalah ya tarawehe itakuwa daima ni yenye kuhimizwa kwa kiasi kikubwa na wala sio faradhi. Hivyo, ‘Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) alianzisha tu kitendo ambacho tayari kilikuwa ni sunnah na wala sio kuanzisha sunnah. Na pia ile sababu ya kutoswaliwa kwa jamaa iliondoka baada ya kuaga dunia kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo hakukukuwa na aina yeyote ya uwezekano wa kuteremshwa wahyi. Na matendo ya makhalifa waongofu pia ni katika sunnah (tizama Hadithi nambari 28 ya al-Arba‘iina an-Nawawiyyah).
Kuhitimisha sehemu hii ya makala haya, ni lazima ieleweke ya kwamba bid’ah si jambo tu jipya ambalo limeanzishwa katika dini kwa dai la kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala), lakini kwa yule mwenye kuanzisha na yule mwenye kufuata bid’ah kwa hakika anatuhumu ya kwamba dini ina upungufu. Hakika ni kuwa wao wanatuonyesha ya kwamba zipo njia za kuja karibu na Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) pamoja na kumridhisha ambako hakupatikani katika Qur-aan au Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na kuwa wao wana njia ya kuamini au kufanya amali na kumuabudu Allaah ambako kunampendeza Yeye na njia mzuri zaidi kuliko zile zilizofundishwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kwamba hii dini ya Uislamu iliyokamilika ina upungufu na hiyo ndio sababu iliyowafanya wao kuongeza baadhi ya vitu au dini hii ina vitu vingi
{Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini}. (5:3)
Na huko ni kukana kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema: “Hakuna kitu ambacho kitakuleta karibu na Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) kuliko yale niliyowaambieni kufanya na hakuna kitakacho wapeleka nyinyi mbali kuliko kufanya yale niliyowakatazeni kufanya”.
Hivyo, tunatakiwa kuchukia bid’ah. Hiki ndicho kiini cha mambo. Uchukivu huu ni kuonyesha mapenzi yetu kwa Allaah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na pia kuipenda dini hii ambayo tunajua na kuwa na yakini kuwa ndio iliyo sahihi kabisa na itabaki hivyo mpaka siku ambayo Allaah Ataibadilisha ardhi hii kwa nyengine.
Madhara (Hatari) ya Bid’ah:
Shaikh Muhammad Sharoot aliandika kuhusu hatari za bid’ah katika kitabu chake na pia naye Dkt. Yusuf Hasan al-Qaradhawi aliandika kuhusu hatari hizi katika kijitabu chake. Shaikh Sharoot anasema ya kwamba lau kama bid’ah ingebanwa kwa yule mwenye kufanya pekee basi huenda hatungefadhaishwa au kubabaika kama tulivyo sasa, lakini hakika ni kuwa hatari za bid’ah na yale madhara na maafa yake yanasambaa kutoka kwa mtu anayefuata na kuwafikia watu wanaoishi naye na mwishowe kwa Ummah mzima. Hivyo, dini kwa ujumla inaathirika kwa ajili ya bid’ah zao na uasi wa kidini. Dkt. Al-Qaradhawi naye anatoa kauli yake kwa kuuliza suali, “Kwa nini Uislamu umeupiga vita vikali jambo hili la bid’ah? Kwa nini Uislamu umeichukulia bid’ah kuwa ni Dhalalah? Kwa nini imemchukulia mwenye kuifanya kuwa ataingia Motoni? Kwa nini Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuonya vikali
1. Mzushi anajiweka katika cheo cha kutunga sheria:
Uhakika ni kuwa Uislamu umetuonya
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاء شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّهُ
“Au hao wana miungu ya kishirikina walio watungia dini asiyo itolea idhini Mwenyezi Mungu?”
(42: 21)
Na kutunga yale yasiyoidhinishwa na Allaah ni hatari kubwa kwa kuwa mwanadamu ameijaalia nafsi yake kuwa sawa na Allaah Aliyetukuka. Na anaona kuwa ni haki yake kuzidisha katika dini ya Allaah, na huu ni mlango ambao huleta hatari kubwa ambayo huwapelekea watu katika shirki na hili ndilo jambo lililoharibu dini kabla.
Dini nyinginezo zilihalalisha nini? Zilihalalisha bid’ah kwa kuifungulia milango na wakajipatia ruhusa na haki ya kuongeza mambo katika dini ya Allaah na wakawapatia haki hiyo makasisi wao au watawa wao. Hivyo dini ikawa si dini na hili ni jambo ambalo Uislamu umelipiga vita vikali, pale Allaah Aliposema:
اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُواْ إِلاَّ لِيَعْبُدُواْ إِلَـهًا وَاحِدًا لاَّ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ
“Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo” (
'Adiy bin Haatim (Radhiya Allaahu 'anhu) aliposilimu baada ya kutoka katika Ukristo (ambao alikuwa akiufuata wakati wa Ujahiliyyah) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikuwa anaisoma aya hii: (
Mzushi hivyo anajipatia cheo cha kutunga sheria na kujiweka sawa na katika upinzani na Allaah Aliyetukuka.
2. Mzushi anaona kuwa dini ina upungufu, hivyo kutaka kuikamilisha:
Watu wa bid’ah wanaona upungufu katika dini nao wakawa wanafanya juhudi ya kuikamilisha katika zile kasoro. Lakini ni jambo ambalo linafahamika na kila Muislamu na hata asiyekuwa Muislamu ya kwamba dini ya Uislamu imekamilika na AllaAh Ametutimizia neema Yake kwa kutukamilishia. Anasema
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينًا
“ Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini” (5: 3).
Imam Maalik (Imam wa ardhi ya Hijrah) alisema: “Yeyote atakayezua katika Uislamu bid’ah ambayo anaiona ni nzuri amedai ya kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefanya hiyana katika kutekeleza ujumbe, kwani Allaah Aliyetukuka anasema, ‘Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini’. Hivyo chochote ambacho hakikuwa dini wakati huo hakiwezi kuwa dini sasa”.
Uzushi katika dini unakuwa ni wenye kumtuhumu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa hakutekeleza jukumu aliloletewa nalo na Allaah. Na Allaah Anasema:
يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ
“Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake” (5: 67).
Dini imekamilika na hivyo haina haja ya kuzidishwa mambo kwani kilichokamilika hakikubali ziada kwa hali yeyote. Kitu chenye upungufu ndicho ambacho kinaweza kuongezwa. Hapa walisimama imara kabisa Masahaba na Maimamu wa Ahlus Sunnah wal Jama’ah na waliowafuata kwa wema dhidi ya bid’ah kwani huko ni kuituhumu dini kuwa imepungua na kumtuhumu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amefanya hiyana.
3. Bid’ah inaifanya dini kuwa nzito na inaitoa katika maumbile yake ya wepesi na usahali:
Dini ambayo imeteremshwa na Allaah ni nyepesi na akatumwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)mwongofu na usahali, uwongofu katika itikadi na wepesi katika taklifu za amali. Allaah Anasema:
يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ
“Mwenyezi Mungu Anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito” (2: 185)
na pia:
وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ
“Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibraahiym” (22: 78).
Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Hakika mimi nimetumwa kufanya sahali mambo na wala sio kuleta uzito wowote” (Imepokewa na al-Bukhaariy kutoka kwa Abu Hurayrah).
Hivyo dini imekuja na usahali kwa watu na wale wenye kuleta bid’ah wanaitoa katika maumbile yake ya wepesi. Hivyo wanawapatia watu taabu na mashaka na wanaongeza vitu ambavyo vinakuwa ni mizigo na minyororo na taklifu kubwa kwa watu. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja kuondoa hiyo mizigo na minyororo iliyokuwa juu ya watu (kwani sheria za zamani zilikuwa ngumu). Allaah Anatufahamisha hayo katika Qur-aan tukufu kwa wasifu wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَآئِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالأَغْلاَلَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ
Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiyesoma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo
Na Allaah Ametufundisha dua ambayo iko mwisho wa Suratul Baqarah ambayo inasema:
رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَآ أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
Hawa watu wa bid’ah wanataka kurudisha ugumu wa dini zilizotangulia katika Uislamu na wanataka kuongeza taklifu ambazo zitakuwa mzigo kwa watu na hivyo kuleta uzito usiotakikana. Taklifu za dini ni sahali na nyepesi
إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا
“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi mlio amini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu” (33: 56).
Na namna bora ya kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni ile aliyotufundisha mwenyewe (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “ALLAAHUMMA SWALLI ‘ALAA
Ewe ndugu yangu katika Imani! Je, kuna dua iliyo nyepesi, nzuri na sahali kuliko dua ambazo zipo ndani ya Qur-aan au Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? Dua ya Qur-aan mfano wa:
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
“Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto!” (2: 201).
Kwa nini tunafanya mambo yawe magumu kwa watu kwa kuwahifadhisha hizo dua badala ya kuwahifadhisha mfano wa dua hii ya Qur-aan?
Al-Qaradhawi anatoa mfano mwengine: “Mara moja nilimwuliza mtu, kwa nini huswali? Akanijibu ya kwamba: ‘Sijui kushika wudhu’. Nikamwambia: ‘Hujui kuosha uso, mikono miwili, kupaka kichwa na kuosha miguu miwili?’ Akasema: ‘Hayo ninajua, lakini sijahifadhi yale yanayosemwa mtu anapoanza kushika wudhu (kutawadha)’. Hiyo ni kusema unapoanza: ‘Alhamdulillahi alladhi ja’alal maa ….’ Unapotia maji puani, ‘Allaahumma arhamni biraihatil jannah …’ Unapoosha uso, ‘Allaahumma bayyidh wajhii…’ na kadhalika mpaka kumaliza. Kila kitu wamekiwekea dua na mtu wa kawaida anaona ili wudhu kuwa sawa ni lazima ulete dua zote hizo ili swalah ipate kusihi. Kwa nini yote haya?”
Nakumbuka nilipokuwa mtoto jinsi ganii katika kisiwa cha Lamu wakati wa Ramadhani watu walivyokuwa wakisumbuka
Uislamu ulisimama imara dhidi ya bid’ah ili watu wasiingie katika mambo mazito na kuongeza vitu ambavyo vitakuwa juu
4. Bid’ah katika dini zinaua (zinaondosha) Sunnah.
Imepokewa kutoka kwa salaf saalih ya kwamba: “Hakuna watu ambao watahuisha bid’ah isipokuwa huondoka mfano wake katika Sunnah”. Hivyo ni kitu kinachoeleweka kuwa hakutaanzishwa bid’ah isipokuwa huchukua nafasi ya Sunnah. Au watu huongeza katika Sunnah mpaka Sunnah ikawa haitekelezwi katika njia yake sahihi. Ibn Abbas anasema, “Pindi bid’ah inapoanzishwa basi Sunnah hutoweka na hii huendelea mpaka bid’ah ikabakia na Sunnah ikatoweka kabisa”. Hasan Ibn Attwiyah, mmoja wa Tabii alisema: “Watu wanapoikubali bid’ah, Allaah huondosha Sunnah kutoka kwao na hairudishi mpaka Siku ya Kiyama”.
Na hili ni jambo la kawaida, nayo ni kanuni, kanuni ya kilimwengu, kanuni ya kijamii.
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ
“Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi” (108: 2)”.
Sikumaliza haya maneno isipokuwa nilimuona shekhe amenikasirikia na kunitoa katika darasa na akaniona mimi ni mtu wa kuleta vurugu na kuwa mimi ninawachukia mawalii na watu wema!
Hii ilinikumbusha mimi ya kwamba hakuna watu wanaohuisha bid’ah na kujishughulisha nafsi zao isipokuwa wanaua sunnah mfano wake na hii ndio siri katika kupinga bid’ah.
Hivyo, bid’ah inaleta chuki kwa Sunnah. Ahl-Bida sio tu wanakataa kuikubali Sunnah sahihi bali pia wanajikataza kwenda katika msikiti au sehemu ambazo Sunnah hutekelezwa.
5. Bid’ah zinaleta mfarakano katika Ummah na kuondoa umoja wao.
Nayo ni kusimama imara katika kutekeleza Sunnah inaleta umoja wa Ummah juu ya kauli moja na hili linawanya Waislamu kuwa safu moja. Lakini bid’ah haimaliziki. Haki ni moja tu lakini batili ina rangi nyingi na aina tofauti. Njia nyoofu ya Allaah ni moja lakini vinjia vya shetani ni vingi
وَأَنَّ هَـذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu” (6: 153).
{Imepokewa na Imam Ahmad, at-Tabari na al-Haakim ambaye ameisahihisha na kukubaliana naye adh-Dhahabi).
Na hivyo Ummah huu uliposhikilia sunnah ilikuwa kauli
Masahaba wote walikuwa msitari wa mbele katika kufuata sunnah za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Walikuwa wanapendana na wakati walipokuwa na tofauti ya ijtihadi baada ya ‘Uthman (Radhiya Allaahu 'anhu) walibaki katika mahaba baadhi
Ummah lau utaachiwa watu wa bid’ah basi hauwezi kuja pamoja, lakini unakuja pamoja tu wakati utasimama nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kufuata Kitabu cha Allaah na Sunnah Zake.
6. Bid’ah ni daraja la kuelekea kwenye Ukafiri:
Mwanachuoni mmoja mkuu, Al-Barbahaari, mmoja wa wanafunzi wa Ahmad Ibn Hanbal, alisema, “Tahadharini bid’ah, kwa sababu kila bid’ah iliyoanzishwa inaanza
Ibn Taymiyyah ameandika kipande kizuri
7. Kwa Ummah wa Kiislamu kwa jumla, bid’ah inarudisha nyuma kuenea Uislamu na Da‘wah kwa ajiili ya Allaah.
Njia na rai za Ahl-ul-bid’ah zinatumiwa na maadui wa Uislamu kuuonyesha Uislamu. Vipindi vingi katika runinga vinaufananisha Uislamu na dhikri ya masufi, matendo ambayo yanakwenda kinyume na Uislamu. Wanaleta mambo
8. Kwa mtu binafsi, bid’ah inaharibu Akhira yake:
Chukua mfano wa mchwa ambao unaruhusiwa kuishi katika ubao. Bid’ah ina athari hiyo hiyo ya
يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا
Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: ‘Laiti tungeli mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungeli mt'ii Mtume!’
وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا
Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.
رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا
Mola wetu Mlezi! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa (33: 66 – 68).
Ufumbuzi wa kujitenga na Bid’ah:
Mwanzo kabisa, watu wanaodai ya kwamba wanafuata Sunnah na kuwa katika msimamo wa Ahl-us-Sunnah Wal Jama‘ah ni lazima waelewe na wafahamu hatari za bid’ah na kuwa ni jukumu la kila mmoja kuchukia na kuipinga. Jambo lolote likifanywa kinyume na Qur-aan na Sunnah ni wajibu wa Waislamu kulikataza jambo kwa njia iliyo nzuri na kuwafahamisha watu madhara ya kwenda kinyume. Kuna mtu aliyekuja kwa Imam Maalik na kumwambia kuwa mimi nataka kuhirimia Madinah. Imam Maalik akamfahamisha kuwa kufanya hivyo ni kinyume na Sunnah kwani ihramu (nia na vazi) inavaliwa katika Miiqaat (sehemu maalumu zilizowekwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Yule mtu akasema kuna tatizo gani na kwa sababu ya umbali kutakuwa na thawabu zaidi. Imam Maalik akamsomea aya ifuatayo:
لَا تَجْعَلُوا دُعَاء الرَّسُولِ بَيْنَكُمْ كَدُعَاء بَعْضِكُم بَعْضًا قَدْ يَعْلَمُ اللَّهُ الَّذِينَ يَتَسَلَّلُونَ مِنكُمْ لِوَاذًا فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Msifanye wito wa Mtume baina yenu
Tuwaite watu kwa njia nzuri kwa busara na mawaidha mazuri. Allaah Anasema:
ادْعُ إِلِى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ
"Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Anayemjua zaidi aliyeipotea Njia Yake, na Yeye Ndiye Anayewajua zaidi walioongoka” (16: 125)
Hapana budi kuanzisha shughuli ya “Amru bil ma‘ruuf wa nahyun anil munkar” (kuamrisha mema na kukataza maovu). Bid’ah ni munkar mkubwa
Ni lazima tutumie fursa ya kuwaelimisha watu na kujifunga sisi wenyewe na Sunnah za kweli za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kutambua mambo ambayo ni bid’ah na yale ambayo si bid’ah. Tufanye bidii kuielewa Qur-aan na pia hadith za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Tujue imani ya kihakika na kufuata maagizo ya Allaah na Mtume Wake. Na ikiwa tunampenda
"Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu." (
Tunamuomba Allaah Atulinde tusiwe ni wenye kufanya bid’ah na Atuongoze katika njia nyoofu na Atusaidie katika kujenga Imani zetu. Mazuri yote yanatokana na Allaah na Mtume Wake na maovu na mabaya yote yanatokana na Shetani na marafiki zake.
“Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo
