Namlea Yatima Wazazi Wake Si Waislamu, Nimsilimishe Kabla Hajabaleghe Au Nisubiri Abaleghe?

 

Namlea Yatima Wazazi Wake Si Waislamu, Nimsilimishe Kabla Hajabaleghe Au Nisubiri Abaleghe?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Nina swali, nini hukmu ya kumlea yatima ambaye wazazi wake si Waislamu. Naweza nikamsilimisha au nisubiri hadi awe na akili zake timamu asilimu kwa hiari yake mwenyewe?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Awali ya yote tunakupongeza kwa utu na ubinadamu wako wa kuweza kumlea mtoto na tunataraji kuwa Allaah Atakupatia thawabu kemkemu kwa hilo.

 

 

Uislamu umemhusisha mtoto mdogo kabla ya kubaleghe na Uislamu. Kwa hiyo, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatueleza: "Kila anayezaliwa anazaliwa katika Fitrah (maumbile ya Uislamu) ila wazazi wake humfanya awe Myahudi, au Mnasara au Mmajusi" [Al-Bukhaariy]. Hivyo, huyo kijana tayari ni Muislamu ni wajibu wako kumfundisha Dini ili awe Muislamu mwema.

 

 

Tunakuombea kila la kheri katika kufanikisha hilo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share