01-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Dibaji Ya Mfasiri

 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu vya Kiislamu vyenye lengo la kuwafahamisha Waislamu Dini yao katika mas-ala ya Ndoa; Ibada na sharia zote za halali na haramu zinazohusiana na maisha ya ndoa.

Nimekichagua kitabu hiki kukifasiri kwa sababu sijaona kitabu kingine kilichoelezea mas-ala ya Ndoa kwa kina na dalili nyingi kama kilivyochambuliwa na kitabu hiki.

 
Ama kwa nini nimeamua kufasiri kitabu kuhusu mas-ala haya; msukumo mkubwa ulionituma kufasiri kitabu katika mas-ala haya ni kuwa leo hii kumekuwa na uharibifu mkubwa katika kufanikisha mas-ala haya ya Ndoa kuanzia inapofungwa Nikaah, karamu, na sherehe zake hadi zinapomalizika Watu wameacha Uislamu na kuridhia mila za kimagharibi, kikabila na mila potofu zinazowatoa Waislamu kwenye Dini yao.

 

Ni maswali mengi yamekuwa yakiulizwa kuhusu mas-ala haya katika mtandao na haswa katika tovuti (website) ya Kiislamu kwa lugha ya kiswahili iitwayo www.alhidaaya.com ambayo yametoa msukumo huo, kadhalika katika kuiendea kazi hii ya mwandishi mwanachuoni wa karne Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy.

 

Hii ni zawadi yangu ndogo kwa mke wangu, wana ndoa wote, wana darsa wangu na wahusika wa Alhidaaya kwa juhudi kubwa za kufanikisha kazi hii.

 
Namuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ajaaliye hiki kitabu kilete manufaa kwa jamii yetu katika mas-ala ya Ndoa na Atutaqabalie hizi juhudi kwa kutujazia katika Miyzaanul-Hasanaat yetu siku ya Qiyaamah.

Abuw 'Abdillaah (3 Rabiy'u Ath-Thaaniy 1428/20 April 2007))

 

Share