09-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuchukua Wudhuu Baina Ya Vitendo Viwili Vya Ndoa

 

 

Mume anapofanya jimai na mkewe katika njia ya halali (ya haki) na akipenda kumrudia mara nyingine (kujimai), basi achukue wudhuu kwanza kutokana na kauli ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم:

 

 ((إِذَا أَتَى أَحَدُكُمْ أَهْلَهُ، ثُمَّ أَرادَ أَنْ يَعُودَ فَلْيَتَوَضَّأ  ْ(بينهما وضوءاً)  ( وفي رواية: وضوءه للصلاة )، فَإِنَّهُ أَنْشَطُ لِلْعَوْدِ))

((Mmoja wenu anapomjia mkewe kisha akipenda kumrudia mara nyingine, basi achukue wudhuu baina ya nyakati (vitendo) mbili (katika riwaaya nyingine wudhuu ule ule kama wa Swalah) kwani hakika itampa (nashati) uchangamfu kurudia kwake))[1]

 



[1] Muslim, Ibn Abi Shaybah na wengineo

Share