39-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuimba Na Kupiga Duff (Matari)

 

 

Inaruhusiwa mume kuwapa ruhusa wanawake katika harusi yake watangaze harusi kwa kupiga duff na kwa nyimbo zinazoruhusiwa tu. Nyimbo ziwe ni zile ambazo hazina maelezo ya uzuri wa maumbile au hazina maneno ya uovu. Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu mas-ala haya:

 


Kwanza:

عن الرُّبيِّعُ بنتُ مُعّوِّذِ بن عفراء: جاء النبيُّ صلى الله عليه وسلم فدخُلُ حين بُنِيَ عليَّ فجلسَ على فِراشي كمجلِسكَ منّي، (الخطاب للراوي عنها ) فجعلتْ جُوَيْرِياتٌ لنا يَضربنَ بالدُفِّ ويَندُبنَ مَن قُتلَ من آبائي يومَ بدرٍ، إذ قالت إحداهنَّ: "وفينا نبيٌّ يَعلمُ ما في غَدِ"، فقال: ((دَعي هذِهِ وقولي بالذيِ كنتِ تقولين))

Imetoka kwa Ar-Rubayy'i ibn Mu'awwidh رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliingia nyumbani kwangu baada ya usiku wa harusi na akakaa katika busati, akiwa karibu kama ulivyokuwa umekaa karibu na mimi (akiwa anamuelezea aliyeisimulia Hadiyth kutokwa kwake). Kisha vijakazi vyetu vya kike vikaanza kupiga duff na kuimba kwa kuwasifu waliouawa katika vita vya Badr". Kisha mmoja wao akasema: "Na miongoni mwetu yupo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye anajua yatakayotokea kesho. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Acheni haya na rudieni kuimba miliyokuwa mkisema kabla ya haya))[1]

 


Pili:

 

عن عائشةَ أنها زَفَّتِ امرأةً إلى رجُلٍ منَ الأنصار، فقال نبيُّ الله صلى الله عليه وسلم: ((يَا عَائِشَةُ! أَمَا كَانَ مَعَكُمْ لَهْوٌ؟ فَإِنَّ الأَنْصَارَ يُعْجِبُهُمُ اللَّهْوُ))

وفي رواية بلفظ : فقال

((فَهَلْ بَعَثْتُمْ مَعَهَا جَارِيَةً تَضْرِبُ بالدُّفِّ وتُغَنِّي؟)) قالت: تقول ماذا؟ قال: ((تقُولُ:

((أَتَيْنَاكُمْ أَتَيْنَاكُمْ

فَحَيُّونَا نُحَيِّكُمْ

لَوْلاَ الذَّهَبُ أَلاحْمَـرُ

مَا حَلَّتْ بِوَادِيْكُمْ

لَوْلا الحِنْطَةُ السَّمْرَاءُ

مَا سَمِنَتْ عَذَارِيْكُمْ))

 

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah الله عنها رضي kwamba alimharakiza? Au Alimsindikiza mwanamke kwa mumewe, siku ya harusi ya mwanamke kwa mume wa ki-Answaar. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamuambia, ((Ewe ‘Aaishah, hukuwa na nyimbo zozote (ulipokuwa unamsindikiza) kwani ma-Answaar wanapenda burudani au viburudisho?))[2]



Na katika riwaaya nyingine ya Hadiyth hii, inasemekana kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alisema, ((Ulimpeleka kijakazi mwanamke pamoja naye kumpigia duff na kuimba?)) Nikamuuliza: Aseme nini (aimbe nini)? Akasema, ((Mwache aseme:


Tumekujieni, Tumekujieni


Kwa hiyo tuamkieni ili tukuamkieni

 
Ingelikuwa sio dhahabu nyekundu


Asingelitwaa katika bonde lenu

 
Na isingelikuwa kwa mtama wa dhahabu

Wasingelinenepa Wanawari wenu))[3]

 

Tatu:

عن عائشةَ رضي الله عنها أَنَّ النبـيَّ سمع ناساً يُغَنُّونَ فـي عُرْسٍ وهم يقولونَ :

وأَهْدَى لَهَا أَكْبُشا  ً يُبَحْبِحْنَ فِـي الـمِرْبَدِ

وحِبُّكِ فـي النَّادِي   ويَعْلَـمُ ما فِـي غَد

وفي رواية:

  وزَوْجُكِ فـي النَّادِي ويَعْلَـمُ مَا فِـي غَدِ، قالتْ: فقالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((لا يَعْلَـمُ مَا فِـي غَدٍ إلاَّ الله سُبْحَانَهُ))  

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliwasikia watu wakiimba katika sherehe ya harusi wakisema:

 

"Na nitampa kondoo wake akichachawa (akirukaruka katika majani kwa furaha) katika karamu – Na mapenzi yako yapo katika klabu, na anajua kesho italeta nini.


Au katika maelezo mengine:

 
Na mumeo yuko katika klabu – Na anajua kesho italeta nini.

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Hakuna anayejua kesho italeta nini (kutatokea nini) isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى))

 


Nne:

عن عامرِ بنِ سعدٍ البَجَلِـيِّ قالَ: دَخَـلْتُ علـى قَرَظَةَ بنِ كعبٍ وأبـي مسعودٍ وذَكَرَ ثالثاً،   ذَهَبَ عَلَـيَّ، وَجَوَارِي يَضْرِبْنَ بالدُّفِّ يُغَنِّـينَ، فقلتُ: تُقِرُّونَ علـى هَذَا وأَنْتُـمْ أصحابُ مـحمدٍ قالُوا: إنَّهُ قَدْ رُخِّصَ لَنَا فـي العُرُسَاتِ والنـياحةِ عندَ الـمُصِيْبَة  .وفي رواية:   وَفِي الْبُكاءِ عَلى الْمَيِّت فِي غَيْرِ نِيَاحَة

Kutoka kwa 'Aamir ibn Sa'ad Al Bajaliy ambaye amesema: "Nilimtembelea Qaradhwah bint Ka'ab na Abu Mas'uud na (akamtaja mwingine ambaye kanitoka), na nikawaona wajakazi wakipiga dufu na kuimba. Nikasema:  Nyote nyinyi mmenyamaza na mnakubali mambo haya na hali nyinyi ni Maswahaba wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم? Wakasema: 'Kwa kweli, alitupa rukhsa ya kufanya haya katika sherehe za harusi na katika wakati wa maombolezo ya msiba".

 

Na katika riwaya nyingine (Wakati wa kilio kwa maiti bila kuwa na maombolezo (yenye kutaja kuhusu maiti na makelele).[4]

 


Tano:

عن أبي بلج يحيى بن سليم قال: قلت لمحمد بن حاطب: تزوجت امرأتين ما كان في واحدة منهما صوت، يعني دفاً، فقال محمد رضي الله عنه: قال رسول الله: ((فَصْلٌ مَا بَيْنَ الحَلالِ والحَرَامِ الصَوْتُ بالدَّفِّ)).

Kutoka kwa Abu Balaj Yahya ibn Saliym ambaye amesema: "Nilimuambia Muhammad ibn Haatwib: Nimeoa wanawake wawili na hakukuwa na sauti (yaani dufu) katika harusi yoyote. Muhammad akasema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema, ((Yanayobainisha baina ya halaal (yaani ndoa za dhahiri) na yaliyoharamishwa (ndoa za siri) ni sauti za dufu))[5]

 


Sita:

قال رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم  : ((أَعْلِنُوا النِّكَاحَ))

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema, ((Tangazeni ndoa))[6]

 



 

 

 



 

[1] Al-Bukhaariy

[2] Al-Bukhaariy

[3] At-Twabaraaniy katika 'Al-Awsatw' Hasan

[4] Al-Haakim, Al-Bayhaaqiy, An-Nasaaiy na wengineo

[5] An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy na wengineo: Hasan

[6] An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy na wengineo: Hasan

Share