SWALAH - 5 - Ni Ibada Muhimu Kabisa

 

 

Swalah ni ibada iliyo muhimu kabisa kuliko amali zote nyinginezo, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuamrisha kwayo mara nyingi katika Qur-aan. Tunazinukuu Aayah chache zifuatazo:

 

Katika mambo ya mwanzo kabisa kutajwa katika Qur-aan kuwa ni miongoni mwa sifa za Waumini watakaofuzu:

 

((الم)) (( ذَلِكَ الْكِتَابُ لاَ رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ))

 

(( الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ))

 

 

((Alif Lam Miym))  

 

 ((Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uongofu kwa wacha Mungu))

 

 ((Ambao huyaamini ya ghayb na hushika Swalah, na hutoa katika tuliyowapa)) [Al-Baqarah: 1-3]

 

 

 

))وَأَقِيمُواْ الصَّلاَةَ وَآتُواْ الزَّكَاةَ وَارْكَعُواْ مَعَ الرَّاكِعِين((َ  

 

((Na shikeni Swalah, na toeni Zakaah, na inameni pamoja na wanaoinama)) [Al-Baqarah: 43]

 

 

  ((فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَ آنْحَرْ))

 

((Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi)) [Al-Kawthar: 2]

 

 

 ((وَاسْتَعِينُواْ بِالصّبْرِ وَالصّلاَةِ وَإِنّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلاّ عَلَى الْخَاشِعِينَ))

 

((Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu)) [Al-Baqarah: 45]

 

 

((حَافِظُواْ عَلَى الصَّلَوَاتِ والصَّلاَةِ الْوُسْطَى وَقُومُواْ لِلّهِ قَانِتِينَ))

 

((Zilindeni Swalah, na khasa Swalah ya katikati, na simameni kwa ajili ya Allaah nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea))) [Al-Baqarah: 238]

 

 

 

((وَأَقِمِ الصَّلاَةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ذَلِكَ ذِكْرَى لِلذَّاكِرِينَ))

 

((Na shika Swalah katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka)) [Huud: 114]

 

 

 

  ((أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآَنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآَنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا))

 

((Shika Swalah jua linapopinduka mpaka giza la usiku, na Qur-aan ya Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri inashuhudiwa daima.)) [Al-Israa: 78]

 

 

 

((فَإِذَا اطْمَأْنَنْتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَوْقُوتاً))

 

((Na mtapotulia basi shikeni Swalah kama dasturi. Kwani hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu)) [An-Nisaa: 103]

 

Wasiya wa Bwana Luqmaan kwa mwanawe:

 

((يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَى مَا أَصَابَكَ إِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ))

 

 

((Ewe mwanangu! Shika Swalah, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa)) [Luqmaan: 17]

 

 

 

Umuhimu Wake Khaswa  

 

 

  1. Ni nguzo ya pili katika nguzo tano za Kiislamu.

 

  1. Jinsi ilivyo muhimu ibada hii hakuna mwenye udhuru nayo; si mgonjwa wala msafiri, hata Muislamu akiwa vitani amewekewa aina yake ya kuswali.

 

  1. Ibada pekee iliyowekewa masharti kama twahara, mavazi na kuelekea Qiblah.

 

  1. Anaposwali mtu, hutumia viungo vyote vya mwili, moyo na ulimi

 

  1. Hairuhusiwi kushughulika kufanya lolote jengine wakati wa kuitekeleza, wala kuzungumza hata kuleta mawazo mengine kwa kujitahidi.

 

  1. Ni kitendo bora kabisa Anachokipenda Allaah kuliko jihaad  pindi akitimiza mja kwa wakati wake:

 

 

 عن أبي مسعود رضي الله عنه قال: سألت رسول الله صلى الله عليه و سلم، أي الأعمال أفضل ؟ قال :

((الصلاة على وقتها))، قلت ثم أي ؟ قال: ((بر الوالدين))  قلت ثم أي؟ قال: ((الجهاد في سبيل الله)) متفق عليه

 

Kutoka kwa Abdullaah bin Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu ambaye amesema: "Nilimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni amali gani inayopendeza kwa Allaah? Akajibu: ((Ni kuswali kwa wakti wake)). Nikamuuliza tena: Kisha ni amali gani? Akajibu: ((Ni kuwafanyia ihsani wazazi)). Nikamuuliza tena: Kisha ni amali gani? Akajibu: ((Ni kupigana Jihaad katika njia ya Allaah)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]

 

 

Itaendelea…/6

 

 

Share