Du'aa Gani Kusoma Unapopatwa na Maumivu Katika Mwili?

 

 Du'aa Gani Kusoma Unapopatwa na Maumivu Katika Mwili?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Assalamu alaykum
 
Mimi nilikuwa namzungumziya jirani yangu kuhusu mtu kama anasehemu inamuuma kisha akaweka mkono wa kulia katika sehemu inamuuma akasema "Bismillahi" mara tatu na kisha akasema " audhu billahia wa kudratih min sharri maa ajidu wa u haadhiru" mara saba inasaiiya kuondowa maumivu. Na yeye akasema ukuwa na maumivi sehemu yoyote kisha ukamswa;iya mtume mara miya na huku ukiwa unapuliziya katika mkono wako kwa kugusa hiyo sehemu inaye kuuma maumuvi yana ondoka. Ma onba kujua kama hya yote ni sahihi? 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Tunakupa kwanza pongezi dada yetu kuwa umeweza kutambua ipasavyo kusomwa hiyo du'aa Muislamu anapopata maumivu katika mwili wake, ingawa umeitaja kwa tamshi. Dalili imekuja katika Hadiyth ifuatayo:

 

 عن عثمان بن أبي العاصأنه شكا إلى رسول الله  صلى الله عليه وسلموجعا يجده في جسده , فقال له رسول الله  صلى الله عليه وسلم: ((ضع يدك على الذي يألم من جسدك وقل : بِسْمِ اللهِ  ثلاثا وقل سبع مرات:   أَعُوذُ باللهِ وَقُدْرَتِهِ مَنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ))  رواه مسلم

Kutoka kwa 'Uthmaan bin Abil-'Aasw kwamba alilalamika kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maumivu aliyopata mwilini mwake, akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Weka mkono wake sehemu inayokuuma katika mwili wako na useme:

بِسْمِ اللهِ 

 mara tatu, kisha sema mara saba:

  أَعُوذُ باللهِ وَقُدْرَتِهِ مَنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ

(Najilinda kwa Allaah na kwa uwezo Wake kutokana na shari ya ninachokisikia na ninachokiogopa) [Muslim]

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate du’aa hiyo pamoja na uweze kuisikiliza kwa sauti:

 

124-Hiswnul-Muslim: Jambo La Kufanya Na Kuomba Du’aa Anaposikia Maumivu

 

 

Ama kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mara mia na kumpulizia, hatukupata dalili katika mafunzo yetu, ikiwa ni kwa ajili ya kuondosha maumivu au hata kwa kutaka tu fadhila zake. Hakuna shaka kwamba kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni ‘ibaadah tukufu na fadhila zake nyingi zimepatikana na ziko tayari mada zake zimeshaandaliwa ndani ya Alhidaaya. Lakini kusema kwamba kumswalia kwa idadi kadhaa na kadhaa na kwa ajili ya kadhaa au kadhaa hatukupata dalili. Kwa hivyo inapasa kujiepusha na mambo yasiyotokana na mafunzo ya Dini yetu khaswa katika hali kama hii ya mgonjwa ili mgonjwa apate haraka kukubaliwa du'aa yake itakayokuwa Swahiyh na si ya uzushi.

 

Tutambue kwamba kuweka idadi ma'aluum katika du’aa bila kuweko dalili katika Qur-aan au Sunnah ni jambo la uzushi (Bid'ah) na linapaswa kuachwa kwani mtu atahangaika bure na kitendo hakitokubaliwa kutokana na dalili za Hadiyth nyingine kuhusu mambo ya Bid'ah, mojawapo wapo ni hii:

 

((من عمل عملا ليس عليه أمرنا فهو رد))     أخرجه مسلم فيصحيحه

((Atakayefanya kitendo kisichokuwa katika amri yetu basi kitarudishwa [hakitokubaliwa])) [Imesimuliwa na Muslim katika Swahiyh yake]

 

Tunamuombea mgonjwa huyo na wagonjwa wote wa Kiislamu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Awape shifaa ya haraka.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share