Zingatio: Amka

                                                                                                                                   
                                                                                          Naaswir Haamid
 
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:(Qiyaamah hakitosimama mpaka mitetemeko ya ardhi izidi) al-Bukhariy
Mengi yameandikwa, mengi tumeyasoma, mengi tumeyasikia. Je, haujafika wakati wa kuamka na kuyazingatia yale ya kutusaidia Siku ya Mwisho? Haijawa bado funzo kwetu kama Qiyama kipo chini ya pua zetu kinasubiri amri tu kije kwetu. Dalili ngapi tushaziona? Dalili ngapi tushazishuhudia? Twasubiri hadi milango ya toba ifungwe ndio turudi kwa Mola wetu? SubhaanaAllaah!
 
Ya Sunami hatuyaoni? yaliyowapata watu Duniani, hadi tukawa mashakani, bado tunamuasi Manani? Tumegeuka ashaddu wa kumuasi ar-Rahmaani, hadi kuwa sawa na nyani? {{Na bila shaka Tumewaumbia Moto wa Jahannamu wengi katika majini na wanadamu: Nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo, na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo. Hao ni kama wanyama; hali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika.}} [Al-A’araaf: 179]
 
Basi kama ndugu yangu Muislamu unazo nyoyo, fahamu umepewa na macho ya kusoma ukaekewa. Nakunasihi uyazingatie haya machache tu yaliyotokea kwa mwaka huu wa 2007[*].

 

TAREHE
SABABU
ENEO
IDADI YA WALIOFARIKI
01/01/07
Ndege iliyokuwa inatoka Java kwenda Manado ilikumbwa na upepo mkali.
Indonesia.
watu 102
02/02/07
Kimbunga
Florida – Marekani
watu 20
19/03/07
Mlipuko wa machimbo ya makaa ya mawe
Urusi
watu 110
01/04/07
Mtetemeko wa ardhi uliwacha maelfu ya watu bila ya makazi na kuuwa
Honiara kwenye Visiwa vya Solomons.
watu 34
05/05/07
Ndege ya Kenya kuanguka kutokana na hali mbaya ya hewa.
Cameroon
abiria wote
24/06/07
kutokana na upepo mkali
Pakistan
Watu zaidi ya 200
17/07/07
Ndege iliyoruka kutoka Uwanja wa ndege ilianguka kutokana na mvua kali
Congonhas
abiria 176
 
 
Tena tutambue haya yote na mengine yanayotokea Allaah Amekwishayaandika na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikwishabainisha kuwa maafa yatakuwa ni mengi karibu na Qiyama: “Saa haitosimama hadi elimu ifutwe, wakati kukimbia kwa kasi, mitetemeko kuzidi kwa sana, fitna kutokea na al-Harj kuengezeka.” Ikaulizwa, “Ewe Mjumbe wa Allaah, nini hiyo al-Harj?” Akasema, “Al Qatl, al Qatl (mauaji)”. [Imepokewa na Imaam Ahmad]
 
Kwa hakika uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya maovu yetu Binaadamu. Na Allaah Anatuonjesha baadhi ya tuliyoyafanya ili tutanabahi na kurudi. {{Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale iliyofanya mikono ya watu, ili Awaonjeshe (adhabu ya) baadhi ya mambo waliyoyafanya, huenda wakarudi (wakatubia kwa Mwenye Enzi Mungu)}}Ar-Ruum 30:41
 
 
Nakunasihi Muislamu kwa mara nyengine tena,
Ghadhabu za Mwenyezi jitahidi kuepukana,
Usije ukatufanya sisi pia maafa kukutana,
Hadi Mola wetu Mtukufu Mkubwa Subhana,
Msamaha Kwake Qiyama tukawa hatuna.
 
Share