Ijumaa: Wanawake Kuswali Adhuhuri Nyumbani Kabla Ya Ijumaa Kuswaliwa

 

SWALI LA KWANZA:

Asalam alykum war hamatu lwah wabarakatu,

Swali:- Swala ya adhuhur katika kipindi hiki cha winter inaingia saa 6 mchana, na wanaume wanaoenda kuswali ijumaa wanaswali saa 7 na robo mchana, kwa hiyo mwanamke anaruhusiwa kuswali kabla ya Ijumaa kuswaliwa? au lazma asubiri mpaka baada ya kuswaliwa ijumaa (saa 7 na robo)

SWALI LA PILI:

assalam alaikum,ningependa kujua kama yafaa kwa mtu ambae hakwenda kuswali mskitini swala ya ijumaa,aweza kuswali adhuhuri wakati waswala ukiingia kabla haija swaliwa ijumaa,au asubiri watu watoke kuswali ijumaa,  assalamalaikum

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa ndugu yetu ambaye ameuliza swali lake hili kuhusu nyakati za Swalah. Nyakati za Swalah ni muhimu kwani Allah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema: “Kwa hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi” (4: 103).

 Swalah kama Ibaadah nyingine ina masharti yake. ili kukubaliwa Ibaadah yoyote ni lazima masharti hayo yawe ni yenye kutekelezwa. Katika mas-ala ya Swalah sharti la msingi la kusihi ni kuingia kwa wakati. Pindi mtu anapokuwa na yakini kuwa wakati huo umeingia basi anafaa kuswali ikiwa yuko peke yake nyumbani au pamoja na familia yake ikiwa ni mwanamme lakini ana udhuru wa kisheria wa kumfanya kutoweza kwenda Msikitini.

Swalah bora kwa wanawake ni kuswali majumbani mwao. Hivyo, pindi wakati wa Swalah yoyote unapoingia ataswali au wataswali bila kungojea ule wakati ambayo Swalah hiyo inaswaliwa Msikitini. Kwa mfano, kulingana na swali Swalah ya Ijumaa huingia saa sita, lakini Msikitini kwa sababu moja au nyingine wanaswali saa saba na robo, wewe unaweza kuswali huo wakati wa awali wa kuingia. Lakini atakapokwenda Msikitini ili apate jamaa itabidi angoje jama'ah yenyewe.

Na Allah Anajua zaidi

 

Share