Saa Ambayo Du'aa Hutaqabaliwa Siku Ya Ijumaa

 

  Saa Ambayo Du'aa Hutaqabaliwa  Siku Ya Ijumaa

 

Alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa utukufu wa Ijumaa ni kuweko saa ambayo du’aa hutaqabaliwa kutokana na dalili:  

   

حديث أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ذَكَرَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَقَالَ: ((فيهِ سَاعَةٌ لاَ يُوَافِقُهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ وَهُوَ قَائمٌ يُصَلِّي، يَسْأَلُ اللهَ تَعَالَى شَيْئًا إِلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ)) وَأَشَارَ بِيَدِهِ يُقَلِّلُهَا       أخرجه البخاري

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitaja kuhusu siku ya Ijumaa na akasema: ((Kuna saa (wakati) katika siku ya Ijumaa ambayo mja Muislamu hatowafikiwa nayo wakati anaswali na anamuomba Allaah  chochote ila Allaah Humpa)) Na  akaashiria udogo wa hiyo saa (huo wakati) kwa mikono yake.   [Al-Bukhaariy]  

 

Je, saa hiyo yenye kutaqabaliwa du’aa   siku ya Ijumaa ni ipi?   

 

'Ulamaa wamekubaliana kuwa ni nyakati mbili kwa dalili zifuatazo:

 

Kwanza: Anapopanda Imaam katika minbari na kukaa kwake hadi anapomaliza Swalaah:

 

عَنْ أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ لِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ: أَسَمِعْتَ أَبَاكَ يُحَدِّثُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي شَأْنِ سَاعَةِ الْجُمُعَةِ؟ قَالَ: قُلْتُ: نَعَمْ سَمِعْتُهُ يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((هِيَ مَا بَيْنَ أَنْ يَجْلِسَ الإِمَامُ إِلَى أَنْ تُقْضَى الصّلاَةُ))

Kutoka kwa Abuu Burdah bin Abiy Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ‘Abdullaahi bin ‘Umar ameniuliza: Je umemsikia baba yako akihadithia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu saa ya [kutakabaliwa du’aa) Ijumaa? Akasema: Nikasema:  Ndio, nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hiyo ni baina ya anapokaa Imaam hadi inapomalizika Swalaah)) [Muslim (853)]

 

Pili: Baada ya Swalaah ya Alasiri hadi kuzama jua. Hii ni kauli inayokubalika zaidi miongoni mwa ‘Ulamaa kwa dalili:

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((يَوْمُ الْجُمُعَةِ اثْنَتَا عَشْرَةَ سَاعَةً ،لاَ يُوجَدُ فِيهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ شَيْئًا إلاَّ آتَاهُ إِيَّاهُ ، فَالْتَمِسُوهَا آخِرَ سَاعَةٍ بَعْدَ الْعَصْر))

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Siku ya Ijumaa kuna masaa kumi na mbili ambayo hapatikani mja Muislamu anayemwomba Allaah kitu ila Anampa, basi itafuteni baada ya Swalaah ya Alasiri".  [Swahiyh Abiy Daawuwd (1048), Swahiyh An-Nasaaiy (1388), Swahiyh Al-Jaami’ (8190)]

 

 

 

 

Share