14-Hadiyth Al-Qudsiy: Jilinde Na Moto Japo Kwa Nusu Tende Au Neno Jema

 

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth ya 14

Jilinde Na Moto Japo Kwa Nusu Tende Au Neno Jema

 

 

عن عَدِيَّ بْنَ حَاتِمٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ يَقُولُ كُنْتُ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَجَاءَهُ رَجُلَانِ أَحَدُهُمَا يَشْكُو الْعَيْلَةَ وَالْآخَرُ يَشْكُو قَطْعَ السَّبِيلِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((أَمَّا قَطْعُ السَّبِيلِ فَإِنَّهُ لَا يَأْتِي عَلَيْكَ إِلَّا قَلِيلٌ حَتَّى تَخْرُجَ الْعِيرُ إِلَى مَكَّةَ بِغَيْرِ خَفِيرٍ وَأَمَّا الْعَيْلَةُ فَإِنَّ السَّاعَةَ لَا تَقُومُ حَتَّى يَطُوفَ أَحَدُكُمْ بِصَدَقَتِهِ لَا يَجِدُ مَنْ يَقْبَلُهَا مِنْهُ ثُمَّ لَيَقِفَنَّ أَحَدُكُمْ بَيْنَ يَدَيْ اللَّهِ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ حِجَابٌ وَلَا تَرْجُمَانٌ يُتَرْجِمُ لَهُ ثُمَّ لَيَقُولَنَّ لَهُ أَلَمْ أُوتِكَ مَالًا فَلَيَقُولَنَّ بَلَى ثُمَّ لَيَقُولَنَّ أَلَمْ أُرْسِلْ إِلَيْكَ رَسُولًا فَلَيَقُولَنَّ بَلَى فَيَنْظُرُ عَنْ يَمِينِهِ فَلَا يَرَى إِلَّا النَّارَ ثُمَّ يَنْظُرُ عَنْ شِمَالِهِ فَلَا يَرَى إِلَّا النَّارَ فَلْيَتَّقِيَنَّ أَحَدُكُمْ النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ فَإِنْ لَمْ يَجِدْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ)) البخاري

Kutoka kwa ‘Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alisema: Nilikuwa kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) na wakamjia watu wawili. Mmoja alikuwa akilalamika umaskini, mwengine akilalamika juu ya uporaji wa njiani. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akasema: Ama kwa uporaji wa njiani, karibu wakati utafika ambapo misafara itaweza kwenda Makkah bila ya walinzi, ama kwa umaskini Saa (Qiyaamah) haitofika kabla mmoja wetu hajachukua swadaqah yake na kuzunguka bila ya kumpa mtu wa kuipokea. Kisha hapo mmoja wenu atasimama mbele ya Allaah bila ya pazia baina yake na Allaah na bila ya mtarujumani (mtu wa kufasiri). Kisha atamuuliza; Je, sikukuletea utajiri? Atasema: Naam. Tena Atasema (Allaah) sikukuletea Rasuli? Atasema: Naam. Ataangalia kulia hatoona chochote isipokuwa Moto, kisha atatazama kushoto hatoona chochote isipokuwa Moto, kwa hivyo muache kila mmoja katika nyinyi ajilinde na Moto japo kwa (kutoa swadaqa) nusu ya kokwa ya tende, na ikiwa hakupata basi kwa (kutamka) neno jema)) [Al-Bukhaariy]

 

Share