17-Hadiyth Al-Qudsiy: Malaika Wanaotafuta Vikao Vya Watu Wanaomdhukuru Allaah Kisha Allaah Huwaghufuria
Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 17
Malaika Wanaotafuta Vikao Vya Watu Wanaomdhukuru
Allaah Kisha Allaah Huwaghufuria
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((إِنَّ لِلَّهِ عَزَّ وَجَلَّ مَلَائِكَةً سَيَّارَةً فُضُلًا يَبْتَغُونَ مَجَالِسَ الذِّكْر، وَإِذَا وَجَدُوا مَجْلِسًا فِيهِ ذِكْرٌ قَعَدُوا مَعَهُمْ فَحَضَنَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا بِأَجْنِحَتِهِمْ حَتَّى يَمْلَئُوا مَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ سَمَاءِ الدُّنْيَا، فَإِذَا تَفَرَّقُوا عَرَجُوا أَوْ صَعِدُوا إِلَى السَّمَاءِ، قَالَ : فَيَسْأَلُهُمْ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ وَهُوَ أَعْلَمُ: مِنْ أَيْنَ جِئْتُمْ؟ فَيَقُولُون:َ جِئْنَاكَ مِنْ عِنْدِ عِبَادٍ لَكَ فِي الْأَرْضِ يُسَبِّحُونَكَ وَيُكَبِّرُونَكَ وَيَحْمَدُونَكَ وَيُهَلِّلُونَكَ وَيَسْأَلُونَكَ، قَالَ: وَمَاذَا يَسْأَلُونِي؟ قَالُوا: يَسْأَلُونَكَ جَنَّتَكَ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: لَا أَيْ رَبِّ، قَالَ: فَكَيْفَ لَوْ قَدْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: وَيَسْتَجِيرُونَكَ ، قَالَ: مِمَّ يَسْتَجِيرُونِي؟ قَالُوا: مِنْ نَارِكَ يَا رَبِّ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا نَارِي؟ قَالُوا: لَا، قَالُوا: وَيَسْتَغْفِرُونَكَ، قَالَ: فَيَقُول:ُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ وَأَعْطَيْتُهُمْ مَا سَأَلُوا وَأَجَرْتُهُمْ مِمَّا اسْتَجَارُوا، قَالَ: فَيَقُولُونَ: رَبِّ فِيهِمْ فُلَانٌ عَبْدٌ خَطَّاءٌ إِنَّمَا مَرَّ فَجَلَسَ مَعَهُمْ، قَالَ: فَيَقُولُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ هُمْ الْقَوْمُ لَا يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ)) البخاري , مسلم , الترمذي والنسائي
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiyy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Aliyetukuka na Jalaali) Anao Malaika chungu nzima ambao wanakwenda huku na kule wakitafuta vikao vya kumdhukuru Allaah; wanakaa na watu hao huku wakikunja mbawa zao baina yao, na kuijaza sehemu ya baina yao na uwingu wa dunia. (Watu) wanapoondoka, (Malaika) hupanda mbinguni. Akasema (Nabiy): Hapo tena Allaah (Aliyetukuka na Jalaal) Huwauliza ijapokuwa Anayajua yote: “Mnatoka wapi?” Wao hujibu: “Tunatoka kwa baadhi ya waja wako duniani, walikuwa wanakusabbih na kukabbir na kuhallil na kukuhimidi na wanakuomba fadhila Zako.” (Allaah) Husema: “Wananiomba nini?” (Malaika hujibu): “Wanakuomba Jannah Yako. (Allaah) Husema: “Wameiona Jannah Yangu?” Husema: “La, Ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Ingekuwaje kama wangaliona Jannah Yangu!?” (Malaika) Husema: “Wanaomba himaya Yako”. (Allaah) Husema: “Wanataka kuhamiwa kutokana na nini kwangu?” (Malaika) Husema: “Kutokana na Moto Wako ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Je, wameuona Moto Wangu?” Husema: “La.” (Allaah) Husema: “Je, ingekuwaje kama wangeuona Moto wangu!?” Husema: “Wanaomba maghfirah Yako”. (Allaah) Husema: “Nimewaghufuria na nimewapa himaya ya yale wanayotaka wahamiwe.” (Malaika) Husema: “Ee Rabb! Miongoni mwao yumo fulani, mja wako muovu ambaye alikuwa akipita tu na akakaa nao”. (Allaah) Husema: “Na yeye (pia) Nimemghufuria. Yule akaaye na watu kama hao hataadhibiwa)) [Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
