Mwanasayansi Wa Kwanza Wa Kiarabu Kuruka Angani Anaitwaje?

 

SWALI:

Mwanasayansi wa kwanza wa kiarabu kuruka angani je anaitwa nani?

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu suala lako.

Hapa tutakujibu swali lako kwa mtazamo wa Kiislam. Na tunadhani umekusudia kuuliza Muislam aliyeruka angani na si Mwarabu. Na hii kama unavyofahamu hii ni tovuti ya Kiislam na haihusiana na ukabila au utaifa, hivyo maswali na majibu yatakuwa yanaendana na muelekeo wa Kidini in shaa Allaah.

Kama tulivyoelezea katika swali lingine kuhusu hatua na maendeleo ya masomo na elimu katika zile ambazo zinajulikana kuwa ni elimu za kisasa. Waislamu tayari walikuwa wamepiga hatua kubwa sana katika elimu za kemia, fizikia, matibabu na upasuaji, historia, jiografia, elimu za sayansi na elimu nyinginezo.

Ama kuhusu mtu aliyeruka inasemekana ni yule aliyejulikana kwa jina la 'Abbaas bin Qaasim bin Firnas. Bwana huyu alizaliwa katika mji wa Ronda, uliopo Andalusia (Spain) mwaka wa 810 Miladi (tarehe za kuanzia kuzaliwa kwa Nabii 'Iysaa). Aliaga dunia mwaka wa 887 Miladi katika mji wa Cordoba, huko huko Andalusia. Hakika ni kuwa pia yeye alibobea katika mas-ala ya utengenezaji wa saa na pia glasi kwa kutumia mawe.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share