Mashairi: Urudi Kwako Nyumbani - Palestina

                      Abdallah Bin Eifan

                  (Jeddah, Saudi Arabia)

Kwa jina la Subhaana, salaamu zipokeeni,

Si usiku si mchana, nawaombea amani,

Inshaallah tutaonana, Al-Quds kama zamani,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Nchi yako Palestina, urudi kwako nyumbani,

Umepata tabu sana, kwa kuishi mahemani,

Washindwe na Maulana, maadui Wazeyuni,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Kwa marefu na mapana, utarejea nchini,

Muhimu kuelewana, chuki acheni pembeni,

Na mzidi kupendana, Awabariki Manani,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Acheni kuchukiana, kamba ya Allaah shikeni,

Ni lazima kupatana, na nia zisafisheni,

Msifanye kugombana, atachochea shetani,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Adui amewabana, sasa miaka sitini,

Hakika mmepambana, ameshindwa kwa yakini,

Walishapata laana, Allah Amewalaani,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Walikuwa ni watwana, Misri kwa Firauni,

Na Musa wakafuatana, na ndugu yake Haruni,

Na kwenye jangwa la Sinaa, Mtume walimkhini,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Hawa ni wabaya sana, na hawana shukurani,

Chakula walitafuna, kilichotoka mbinguni,

Walizidi kutukana, na kuasi ardhini,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Wanapenda ufitina, na ujeuri kichwani,

Waliomba Kumuona, Allaah machoni,

Kaghadhabika Rabbana, wakateseka jangwani,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Wao ukweli hawana, uongo ni yao dini,

Kwa hivyo tumeshaona, nia yao ya moyoni,

Na wanasaidiana, pamoja na Marekani,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Umoja sisi hatuna, chunguza mikutanoni,

Tunabaki kubishana, faida hatuioni,

Lazima kushikamana, kwa subira na imani,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Na Allaah Anatuona, Ametupa mtihani,

Kwa hivyo tuombe sana, rehema za Rahmani,

Nimemaliza kunena, hapa mwisho wa maoni,

Urudi kwako nyumbani, nchi yako Palestina.

Share