038-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Wajibu Wa Kutulia Katika Sujuud Na Adhkaar Za Sujuud

 

WAJIBU WA KUTULIA KATIKA SUJUDU

 

Alikuwa ( (صلى الله عليه وآله وسلمakiamrisha kutimiza rukuu na sujuud, na akimlinganisha mtu asiyetimiza hivyo kuwa ni kama mtu mwenye njaa anakula tende moja au mbili ambazo hazimsaidii kitu cho chote. Pia akimuambia kuhusiana na asiyetimiza: ((Hakika yeye ni muovu kabisa miongoni mwa watu  wezi)).

 

Vilevile alikuwa ( (صلى الله عليه وآله وسلمakihukumu kubatilika kwa Swalah ya mtu asiyenyoosha mgongo wake sawa sawa katika rukuu na sujudu, kama ulivyotangulia uchambuzi wake katika rukuu, na akamuamrisha aliyeswali vibaya atulie katika sujuud, kama ilivyotangulia katika mlango wa kwanza.

 

 

 

ADKHAAR ZA SUJUDU

 

Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema katika nguzo hii namna mbali mbali za adhkaar na du'aa zozote, mara hizi na mara nyingine hizi. Kati ya du'aa hizo ni hizi zifuatazo:

 

1.

 

Subhaana Rabbiyal ‘Alaa

Ametakasika Mola wangu Aliye juu. (mara tatu).( [1])

 

 

Mara nyingine aliikariri zaidi ya mara hizo.([2])

 

 

Mara moja aliikariri sana katika Swalah ya usiku hadi sujuud yake ilikuwa inakaribiana na kisimamo chake alichokuwa amesoma ndani yake Surah tatu katika Surah ndefu; Al-Baqarah, An-Nisaa na Al-'Imraan. Ndani yake (Swalah hii) kulijaa du'aa na kuomba maghfirah, kama ilivyotajwa kabla katika Swalah ya Usiku.

 

 

2-

 

 

Subhaana Rabbiyal ‘Alaa wabihamdihii

Ametakasika Mola wangu Aliye juu Na Sifa Njema Ni Zake. (mara tatu)([3]).

 

 

3-

 

Subuuhun Qudduusun Rabbul Malaaikati war Ruuh

Mwingi wa kutakaswa Mtakatifu, Mola wa Malaika na Jibriyl.([4])

 

 

 

 

4-

 

 

Sub-haanaka Allaahumma Rabbanaa wa Biham-dika Allaahumma gh-fir-liy

Kutakasika ni Kwako, Ewe Allaah! Mola wetu, na sifa njema zote ni Zako, Ewe Allaah! Nisamehe.

Alikuwa akiileta kwa wingi hii katika rukuu yake na sujuud zake, alikuwa akitekeleza amri ya Qur-aan.([5])

 

 

5-

 

 

Allaahumma laka Sajad-tu, wabika Aamantu, walaka As-lamtu, [Anta Rabbiy] Sajada wajhiy Li-lladhiy Khalaqahu waswawwarahu, [fa-ahsana swuwarahu] washaqqa sam’ahu wabaswarahu, [fa]tabaaraka Allaahu Ahsanul Khaaliqiyn.

Ee Allaah! Kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimesilimu, (Nawe ni Mola Wangu) umesujudu uso wangu kumsujudia Yule Aliyeuumba na Akautia sura, na Akaupasua usikizi wake na uoni wake, [Basi] Ametukuka Allaah Mbora wa waumbaji.([6])

 

 

6-

 

 

Allaahumma gh-firliy dham-biy kullahu, wa diqqahu, wajillahu, wa awwalahu wa aakhirahu, wa’alaaniyyatahu wasi-rrahu.

Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za siri.([7]) 

 

 

7-

 

 

 

 

Sajada laka sawaadiy wakhayaaliy, wa aamana bika fuaadiy, abuu-u bini’matika ‘alayya, haadhay yadayy wamaa janaytu ‘alaa nafsiy.

Utu wangu na kivuli changu kimekusujudia, moyo wangu umekuamini, nakiri neema Zako kwangu, hii ni mikono yangu na yote niliyochuma dhidi yangu.([8])

 

 

8-

 

 

 

Subhaana dhil Jabaruuti wal Malakuuti wal Kibriyaau wal ‘Adhwamati

Ametakasika Mwenye Utawala, na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu([9]). Hii alikuwa akiisema katika Swalah ya usiku pamoja na zifuatazo:

 

9-

 

 

Sub-haanaka [Allaahumma] wabihamdika, La ilaaha illa Anta

Kutakasika ni Kwako, (Ee Allaah) na sifa njema ni Zako, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.([10])

 

 

10-

 

 

Allaahumma gh-firliy maa Asrartu, wamaa a’lantu

Ee Allaah! Nisamehe (dhambi) nilizofanya kwa siri, na (dhambi) nilizofanya dhahiri.([11])

 

 

 

11-

 

 

 

Allaahumma j-‘al fiy qal-biy nuura, [wafiy lisaaniy nuura], waj-‘al fiy sam’iy nuura, waj-‘al fiy baswariy nuura, waj-‘al min tahtiy nuura, waj-‘al min fawqiy nuura, wa’an yamiyniy nuura, wa’an yasaariy nuura, waj-‘al amaamiy nuura, waj-’al khalfiy nuura,[waj-‘al fiy nafsiy nuura], wa-a’dhim liy nuura.

Ee Allaah! Jaalia nuru katika moyo wangu, [na katika ulimi wangu nuru], na Jaalia katika masikio yangu nuru, na Jaalia katika uoni wangu nuru, na Jaalia chini yangu nuru, na Jaalia juu yangu nuru, na kulia kwangu nuru, na kushoto kwangu nuru, na Jaalia mbele yangu nuru, na Jaalia nyuma yangu nuru (na Jaalia katika nafsi yangu nuru), na Nifanyie kubwa nuru.([12])

 

 

12-

 

 

Allaahumma [Inniy] A’udhuu biridhwaaka min sakhatwika, [wa A’udhuu] bimu’aafatika min ‘uquubatika, wa’Audhuu Bika Minka, laa uhswiy thanaa-an ‘alayka Anta kamaa Ath-nayta ‘alaa Na-fsika

Ee Allaah! Hakika [mimi] najilinda kwa Radhi Zako kutokana na hasira Zako, na [najikinga] kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najilinda Kwako Unihifadhi na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe.([13])

 

 

 

 





[1] Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwniy, Atw-Twahaawiy, Al-Bazzaar na Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr kutoka kwa Maswahaba saba. Taz. Pia Tanbihi katika Adhkaar za Rukuu.

[2] Taz. Tanbihi katika Rukuu pia.

[3] Swahiyh, imesimuliwa na Abu Daawuud, Ad-Daaraqutwniy, Ahmad, At-Twabaraaniy na Al-Bayhaqiy.

[4] Muslim na Abu 'Awaanah.

[5] Al-Bukhaariy na Muslim.

[6] Muslim, Abu 'Awaanah, Atw-Twahaawiy na Ad-Daaraqutwniy. 

[7] Muslim na Abu 'Awaanah.

[8] Ibn Naswr, Al-Bazzaar na Al-Haakim, aliyekiri kuwa ni Swahiyh lakini Adh-Dhahabiy hakukubali. Hata hivyo, inayo nguvu ambayo imetajwa katika toleo la muswada. 

[9] Abu Daawuud na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Muslim, Abu 'Awaanah, An-Nasaaiy na Ibn Naswr.

[11] Ibn Abi Shaybah (62/112/1) na An-Nasaaiy; Al-Haakim amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekubali.

[12] Muslim, Abu 'Awaanah na Ibn Abi Shaybah (12/106/2, 112/1).

[13] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

Share