Damu Inayotoka Akiwa Mja Mzito Ni Kama Ya Hedhi Je Aswali?
SWALI:
Asalamu Alaykum: Mimi ndugu yenu muislam nina suali langu linanipa utata naomba ufafanuzi kutoka kwenu. Suali langu ni hili:-
Hivi mtu akiwa mja mzito akawa anablid mara kwa mara na damu inatoa harufu
Naomba kujibiwa.
Ahsante.
JIBU:
AlhamduliLLah, Waswalaatu Was-salaam 'alaa Rasuli-Llah صلى الله عليه وآله وسلم Amma ba'ad,
Damu inayomtoka mwanamke anapokuwa mja mzito inaweza kuwa ni damu ya hedhi au damu ya kawaida au inaweza kuwa ni damu ya nifaas ikiwa ni karibu na kuzaa.
Kutokana na ulivyoeleza kuwa unapata damu na inatoa harufu kama ya hedhi basi bila shaka hiyo itakuwa ni hedhi, kwani Maulamaa wamekubaliana kuwa damu huwa damu ya hedhi ikiwa itakuwa na sifa za damu ya hedhi. Hivyo itabidi uache kuswali na kufunga.
Rai ya kwamba mwanamke mjamzito anaweza kupata hedhi ni rai ya madhehebu ya Imaam Shaafi'i ambayo imesimuliwa kutoka Imaam Ahmad. Na vile vile imewafikiwa na Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyah, lakini ni jambo la nadra
Rai ya Shaykh Muhammad bin 'Uthaymiyn ni kwamba, damu huwa ya hedhi ikiwa itakuwa na sifa za damu ya hedhi na hutokea wakati ule anaoutarajia mwanamke
Na huwa ni damu ya kawaida ikiwa haina sifa za damu ya hedhi au damu ya nifaas, yaani rangi yake huwa nyekundu na hii huwa ni 'istihaadhah' (Damu ya hedhi itokayo muda au siku zisizotarajiwa). Na hii ndio inayoitwa 'An-naziyf' (lit. haemorrhage)
Wa Allaahu A'alam
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


