Nini Maana Ya Manhaj Ya Salafiyyah?

 

Nini Maana Ya Manhaj Ya Salafiyyah?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini maana ya (al.manhajusalafiya) na je ni kikundi ao ni dini mpya. Nifidisheni mungu akulipeni fiduniya wal akhera

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Haya ni maneno mawili ambayo si mageni kwani yanatumika sana katika Lugha ya Kiarabu. Neno la kwanza Manhaj ina maana ya muongozo, njia au mfumo wa kitu chochote kile. Ama neno la pili Salafiyyah ina maana ya watangu au waliopita. Hivyo, kiujumla maneno hayo mawili yana maana ya muongozo ulioachwa na watu wema waliopita kama Swahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wale waliowafuata kwa wema.

 

Hii si Dini mpya ambayo imekuja kwetu kwani Dini yetu ya Uislamu haibadiliki mpaka siku ya Qiyaamah. Kwa kuwa Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) ndio walioifahamu Dini hii ya Uislamu zaidi kuliko waliokuja baada yao. Hivyo, wale Waislamu waliokuja baada yao walijifunza kutoka kwao na kizazi baada yao kikajifunza kutoka kwa waliopita mpaka ikatufikia sisi kwa njia nzuri na safi kabisa.

 

Na wanaofuata Manhaj hii wanajulikana zaidi kwa jina la Ahlus Sunnah wal Jamaa'ah au Salafi.

 

Kwa hiyo, hiki si kikundi wala Dini kando bali ni muongozo aliokuja nao Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ukafahamika na kufuatwa na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata hao kwa wema hadi Qiyamaah. Ni Muongozo wa Dini yetu hii ya Uislamu, ambao utakupatia ufanisi hapa duniani na kesho Aakhirah.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share