Mume Aliyemdhulumu Mtalaka Wake Haki Zake. Anasema Akiomba Toba Basi Atasamehewa Na Allaah. Je, Vipi Mke Atalipwa Haki Yake?

SWALI:

 

Asalaam alaikum warahmatulahi wabarakatu. Mwanamume alie mdhulumu mtalaka wake haki zake zote za kinyumba kwa jumla kama inavyostahiki mume kumuangalia mkewe, kisha yule Mume kasema kuwa akiomba toba kwa Mola wake ataswamehewa. Jee yule Mke alie dhulumiwa auliza atalipwa vipi na Allah na Mtalaka wake kashaomba toba? Hii kesi mbele ya Allah itaamuliwa vipi ikiwa mume aliedhulumu itakubaliwa toba yake? Shukran.

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu dhulma aliyofanyiwa mke na mtalaka wake. Ama swali hilo halina utata kabisa kwani Uislamu umetupatia ufumbuzi wa kila kitu.

 

Moja wapo ya hayo mambo ni masharti ya toba kwa mtu aliyefanya makosa. Masharti yenyewe ni kama yafuatayo:

 

1.     Kuacha maasiya.

 

2.     Kujuta katika kufanya hayo maasiya.

 

3.     Kuazimia kutorudia makosa hayo.

 

4.     Akiwa amemkosea mwanaadamu mwenziwe basi aombe msamaha kutoka kwake.

 

Kwa sharti la nne huyo mtalaka wake kusamehewa mpaka yeye amsamehe. Ikiwa hatomsamehe basi Allaah Aliyetukuka Atamlipa kwa kuchukua mazuri yake na kumpatia yeye Siku ya Qiyaamah. Tufahamu Allaah Aliyetukuka ni Muadilifu na hapendi dhulma kabisa na dhulma itakuwa giza kwa mwenye kuifanya Siku ya Qiyaamah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share