Asiye Muislamu Anaweza Kuingia Msikitini Kufanya Matengenezo?

SWALI:

 

Assalaam Alaykum Warahmatul Laahi Wabarakat, Ama Baad, Mashehe zetu tunakuuombeni kila la kheri na kwa sote waumin wa kiislam, Suala langu, jee mtu asiekua muuislam kwa mfano kama mkristo ambaye ni fundi wa umeme na mimi namhitaji anifanyie matengenezo ndani ya msikiti wetu, inafaa mtu huyo nimuingize ndani ya msikiti kwa ajili ya matengenezo na hali yakua si muuislam na la pili namuuogopa Allaa kwa kufanya hivo kwa kuhofia mwili wake una janaba kwa kua hana iitikadi ya kiislam. shukran.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu asiyekuwa Muislamu kuingia Msikitini kwa ajili ya kutengeneza au kufanya ukarabati.

Hakika hakuna tatizo kabisa kufanya hilo kwani wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaruhusu wasio Waislamu kuingia Msikitini. 

 

Na hiyo pia ni njia moja ya kuwalingania wasiokuwa Waislamu waone Msikiti ulivyo tofauti na nyumba zao za ‘Ibaadah. Na pia hiyo ni fursa ya kumueleza yeye juu ya Uislamu. Kuchungwe usafi na stara.

 

Lakini, hata hivyo ni bora na muhimu zaidi kumpatia kazi hiyo Muislamu ili apate chochote cha kuweza kujikimu nacho kimaisha.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share