050-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Qunuut An-Naazilah Katika Swalah Tano (Qunuut Wakati Waislamu Inapowafikia Janga, Au Maafa)

Qunuut An-Naazilah Katika Swalah Tano (Qunuut Wakati Waislamu Inapowafikia Janga, Au Maafa)

 

Alipotaka   (صلى الله عليه وآله وسلم) kuomba dhidi ya mtu, au kumuombea mtu, alifanya Qunuut ([1]) katika Rak’ah ya mwisho baada ya rukuu, na baada ya kusema: 'Sami'a Allaahu Liman Hamidah, Allaahumma Rabbana lakal Hamd’([2]) "Aliomba kwa sauti"([3]) "alinyanyua mikono"([4]) "ya walionyuma yake walisema Aamiyn"([5])

"Alikuwa akifanya Qunuut katika Swalah zote tano"([6])lakini "hakuwa akifanya Qunuut humo ispokuwa alipoomba dhidi ya watu au kuwaombea watu"([7]) Mfano, mara alisema: ((Ee Allaah! Muokoe Al-Waliyd Ibn Al-Waliyd na Salamah Ibn Hishaam na 'Ayyaash Ibn Abi Rabiy'ah. Ee Allaah! Zidisha adhabu Yako kwa (kabila la) Mudhwar, na wajalie miaka (ya ukame) kama miaka ya Yuusuf. [Ee Allaah! Malaani Lahyaan na Ru'lan, na Dhakwaan, na 'Uswayyah waliomuasi Allaah na Mjumbe Wake]))([8])

Kisha "alikuwa akisema: 'Allaahu Akbar' anapomaliza Qunuut na kusujudu"([9])

 [1] "Qunuut" inabeba maana nyingi kama unyenyekevu na uchaji. Na

ilivyokusudiwa hapa ni du'aa khaswa wakati wa kusimama katika Swalah.

[2] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[3] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[4] Ahmad na Atw-Twabaraaniy ikiwa na isnaad Swahiyh. Kunyanyua

mikono katika qunuut ni madhehebu ya Ahmad na pia Is-haaq bin Raahawaih kama ilivyo katika Masaail ya Al-Marwazy (Uk. 23). Ama kufuta uso kwa mikono, hili halikuripotiwa katika hali hii, hivyo ni bid'ah. Ama nje ya Swalah, haikusimuliwa kuwa ni Swahiyh. Yote yaliyosimuliwa kuhusu hili, ni dhaifu au dhaifu sanakama nilivyohakikisha katika Dhwa'iyf Abu Daawuud (2) na Silsilatul-Al-Ahaadiyth As-Swahiyhah (597). Hii ndio maana Al-'Izz bin 'Abdus-Salaam amesema katika fatwa zake, "Mtu mjinga tu ndiye anayefanya" Taz. Kiambatisho 8.

[5] Abu Daawuud na Siraaj. Al-Haakim amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy na wengineo wamekubali.

[6] Abu Daawuud, Siraj na Ad-Daaraqutniy ikiwa na isnaad mbili Hasan.

[7] Abu Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/78/2) na Al-Khatwiyb katika Kitabu Al-Qunuut ikiwa na isnaad Swahiyh.

[8]  Al-Bukhaariy na Ahmad, ziada kutoka kwa Muslim.

[9] An-Nasaaiy, Ahmad, Siraaj (109/1) na Abu Ya'laa katika Musnad yake ikiwa na isnaad nzuri.

Share