Kutoa Damu Kunavunja Swawm?
SWALI:
asalam alaykum,
suali langu ni hili jee kama mtu amefunga na akaenda hospital akatolewa damu ktk mkono wake kidogo ktk vichupa
Jazaka llahulkheir
JIBU:
Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza tunatoa shukurani kwako kwa kutuma Swali lako hili ukiwa umeweka maudhui yake iliyo wazi kabisa, jambo ambalo hutufanyia wepesi sisi kuweza kulipata swali tunapotaka kulijibu haraka. Tunaomba ndugu zetu wengine wote watimize utaratibu huu muhimu. Jazaaki Allahu Khayra.
Shukran kwa swali lako zuri kuhusu mas-ala ambayo ima hufungua saumu ya mtu au hayafungui. Katika mas-ala tuliyo nayo hapa ni kutoa damu kidogo na kutiwa katika vichupa
Kwa Hadithi hii wanazuoni wamesema ikiwa kutoa damu kule kutamdhoofisha Muislamu na kumtia taabuni basi ni afadhali afungue lakini ikiwa anaona ni sawasawa wala hana shida yoyote basi anaweza kuendelea kufunga na saumu yake itakuwa inasihi.
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
