13-Wasiya Wa Mwisho Wa Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Katika Amri Yake ya Mwisho, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Alitukataza Kufanya Jambo Moja tu; Bid’ah

 

Katika Amri Yake ya Mwisho, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Alitukataza Kufanya Jambo Moja tu; Bid’ah.

 

Iwapo mtu anaweza kufikiria maneno ya Mtume katika maamrisho ya mwisho, mtu atagundua ya kuwa amri za kufanya zinazidi makatazo, ambayo inahesabika kuwa yule anayeshikamana na Sunnah, hahitaji ufafanuzi kuhusu njia za upotofu –Amri za kufanya ni hizi hapa:

 

1.     Mche sana Allaah

 

2.     Sikiliza na tii

 

3.     Jihimize kufanya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Sunnah za Makhalifah waongofu.

 

Ama kuhusu makatazo, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hapa alitukataza jambo moja, alisema, “Jihadharini na muwe mbali na mambo yaliyozuliwa”, ambayo inaelezea au inaashiria: kaeni mbali na mambo mapya na yaliyozuliwa, na matokeo yake mtaokolewa na kufanikiwa. Bid’ah ni siri iliyopo nyuma ya upotofu, kukengeuka na upotevu kamili, kwani inapelekea na wakati mwingine inahusu shirki na ukafiri. Kwa hiyo yeyote anayefunga mlango wa uzushi ameongozwa kwa ridhaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Kuhusu bid’ah, mtu anatakiwa azingatie Hadiyth hii:

“Kwa hakika, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amezuia toba ya mwenye kufanya kila bid’ah.”[1]

 

 

 

Hitimisho

 

Kwa hakika, amri ya mwisho ya Mtume ilikuwa sawa na khutbah zake: zilisababisha mioyo kutetema na macho kububujika machozi, lakini zikiacha mioyo na macho aminifu. Mioyo inatetema kwa sababu ya madhila tunayoyapata ukilinganisha na heshima tuliyoisikia. Macho yanabubujika machozi kwa sababu ya kuparaganyika Waislamu na kwa sababu ya kugawanyika miongoni mwao, ambayo imetusibu baada ya kipindi cha utukufu, heshima na uongozi.

 

Hata hivyo kuna matarajio: maamrisho ya mwisho yana mambo yanayoweza kutuokoa na madhila tuliyomo. Kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), vita kuhusu utashi, kushikamana na Sunnah za Mtume na Sunnah za Makhalifah waongofu, uelewa sahihi wa Qur-aan na Sunnah, ambayo inaambatana na uelewa wa Maswahaba;  na kutojihusisha na bid’ah – yote  haya yamo katika amri ya mwisho ya Mtume. Shikamana na maamrisho hayo na ng’ata kwa magego yako (Allaah Awe radhi nawe) ili uwe miongoni mwa wale watakaokombolewa, wale waliofuzu, kwa ridhaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).[1] Ilisimuliwa na Abu Ash-Shaykh, katika “At-Taariykh Asbahaan,” na At-Twabaraaniy katika “Al-Awsatw”, na wengineo. Rejea “As-Swahiyhah (1620).”

 

Share