Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ya Ng’ombe

Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ya Ng’ombe

 

Vipimo

Ndizi - 15 takriiban

Nayma ya ng’ombe - 1 kilo

Kitunguu maji - 1

Nyanya - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu

Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilopondwa - 2

Jira/cummin/bizari ya pilau ilosagwa - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 1

Chumvi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha nyama kwa ndimu, chumvi na tangawizi mbichi na kitunguu thomu.
  2. Menya ndizi na zikatekate vipande kiasi, weka katika sufuria.
  3. Katakata kitunguu na nyanya utie katika ndizi.
  4. Tia jira na chumvi.
  5. Nyama ikiwiva mimina pamoja na supu yake ufunike ndizi ziwive na kuwa tayari kuliwa.
  6. Ukipenda tia pilipili mbuzi zichemke pamoja na ndizi.

 

Share