Zingatio: Allaah Wanusuru Ndugu Zetu Wa Dammaaj Wanaouawa Na Mashia

 

Zingatio: Allaah Wanusuru Ndugu Zetu Wa Dammaaj Wanaouawa Na Mashia

 

Na: Naaswir Haamid

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Hali inayoendelea nchi za Waislamu na zaidi kwa Mashariki ya Kati sio yenye kuridhisha. Huenda ikawa ni kwa sababu za kisiasa, kiuchumi au kijamii zimesababisha machafuko haya yote kutokea. Lakini kikubwa zaidi ni kukosekana imani thaabit na mashirikiano kama tulivyofunzwa katika misingi ya Kiislamu.

 

 

Matokeo yake ndio hayo, hivi sasa ndugu zetu wa Dammaaj huko Yemen wanavamiwa na kuteswa na Mashia kwa sababu ya ‘Aqiydah yao na misimamo yao. Eneo la Sa’ada Dammaaj lenye makaazi ya taasisi ya kiielimu inayoitwa Daarul-Haadiyth lina wakaazi wapatao 10,000 na familia 3,000; kwa masikitiko hivi sasa eneo hili limezungukwa kwa vifaru na wanajeshi wanaoongozwa na Mashia wenye asili ya Hawthi. Ndugu hawa wa Dammaaj hawaruhusiwi kupatiwa msaada wa chakula wala kimatibabu kwa muda sasa.

 

 

Mashambulizi hayo yameshtadi zaidi katika siku za hivi karibuni, ambapo Mashia hao walipanda mlima na kuanza kuwashambulia wakaazi hao. Hata hivyo, watu wa Dammaaj kwa uwezo wa Allaah wameweza kujihami na kukabiliana na kundi hilo linaloongozwa na Mashia, na imeripotiwa kuwa takriban wanafunzi kadhaa wameuawa na Mashia na wengine wamejeruhiwa vibaya mno wakiwemo wanafunzi kutoka nchi za Ulaya, Marekani, Asia na kwengineko. Hata hivyo ndugu zetu kwa msaada wa Allaah wanakabiliana na Mashia hao walio wengi kwa idadi na silaha na kuweza kwa tawfiyq ya Allaah kuwajeruhi wengi na hadi kufikia kwamba hospitali ya Sa’dah kutoweza kuwamudu mahututi hao. Kwa hakika, ndugu zetu wa Dammaaj wameifanyia kazi kauli ya Allaah:

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ فَانفِرُوا ثُبَاتٍ أَوِ انفِرُوا جَمِيعًا ﴿٧١﴾

71. Enyi walioamini! Shikeni hadhari yenu; tokeni kwa vikosi vikosi au tokeni kwa pamoja[An-Nisaa: 71]

 

 

Na pale Aliposema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿١٢٣﴾

123. Enyi walioamini! Piganeni jihaad na wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.” [At-Tawbah: 123]

 

 

Naye Nabiy wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba: “Hapana kuhajir tena (kutoka Makkah kwenda Madiynah) baada ya Waislamu kuuteka (mji wa Makkah) isipokuwa (kilichokuwepo ni) Jihaad na niyyah (ya kupigana Jihaad), na mnapoitwa muitikie (mwito).”  [Imepokewa na Al-Bukhaariy].

 

 

Halikadhalika, makundi ya Waislamu yenye msimamo sahihi madhubuti wenye kufuata Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Halikadhalika, Wanachuoni kadhaa wamekubaliana kwamba Dammaaj ina haki ya kujilinda na kuihami jamii yake katika watoto, wake na mali zao.

 

 

Cha kustaajabisha ni namna vyombo vya habari vilivyojifanya kuwa bubu na viziwi juu ya uvamizi huo wa Maraafidhah kana kwamba hakuna mapigano. Habari zinazotoka Dammaaj ni zaidi kutoka kwa wapenda kheri kwa njia ya simu na mitandao mengine.

 

 

Lakini Rahma za Allaah ni kubwa na hakika Atawanusuru wale waliokuwa wakimukhofu hapa duniani kwa siri na dhahiri na Atawaacha waovu wakiwa wenye kukhasirika:

 

ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا ﴿٧٢﴾

72. Kisha Tutawaokoa wale waliokuwa na taqwa, na Tutawaacha madhalimu humo wamepiga magoti. [Al-Maryam:72]

 

 

Hivyo, nasi tujihimu kufuatilia ukweli uko wapi, kushuhudia unyama wanaoufanya Mashia dhidi ya Dammaaj na halikadhalika kuwaombea dua’a ndugu zetu hawa; Allaah Awapatie nguvu na ushindi madhubuti utakaowajaalia kupata radhi za Allaah duniani na Aakhirah pamoja na kuwajaalia kurejea maisha yao kama yalivyo awali. Na tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awaangamize Raafidhwah -maadui wakubwa wa Uislamu- popote walipo. Aamiyn

 

Share