25-Swabrun Jamiyl: Subira Za Taabi'iyn - Sa'iyd Bin Musayyib (Rahimahu Allaah)

 

Swabrun Jamiyl (Subira Njema)  

 

25 - Subira Za Taabi'iyn - Sa'iyd Bin Musayyib (Rahimahu Allaah)

 

 

 

Sa’iyd bin Al-Musayyib (Rahimahu Allaah) aliishi maisha ya hali nzuri na alikuwa mwenye hadhi. Hakuwahi kuinamisha kichwa chake kwa mtu yeyote yule, hata kama atapigwa kwa mijeledi au kutishiwa kuuwawa.

 

Hali hiyo ndio iliyomfikia  kutoka kwa Amiyr wa Madiynah katika Ukhalifa wa ‘Abdul-Malik bin Marwaan akimuamuru amfanyie bay’ah (kiapo cha utii) Waliyd bin ‘Abdil-Malik. Alipokataa Sa’iyd kutii kiapo hicho, alitishwa kuuawa. Lakini hakurudisha rai yake pamoja na elimu yake na yale yanayomsubiri na adhabu. Sa’iyd alipoonesha kukataa kwake, walimvua nguo zake na wakampiga mboko hamsini, na wakamzungusha katika soko za Madiynah wakiwa wanasema: “Hii ndio hali ya mwana hezaya!” Sa’iyd akiwajibu huku akijiamini kwa kusema: “Bali ni nani mwana hezaya basi turudishe kwa lile tunalotaka.”

 

‘Abdul-Malik alipojua kilichofanywa na Walii wake wa Madiynah, alimlaumu na akamwandikia:  “Wa-Allaahi, ilikuwa mpate huruma kutoka kwake Sa’iyd, na sio kumpiga, nami najua tofauti iliyopo na kupinga kwake.”

 

Share