Shaykh Fawzaan: Nasaha Kwa Waislamu Kutulia Kuhusu Filamu Ya Kumkashifu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Nasaha Kwa Waislamu Kutulia Kuhusu Filamu Ya Kumkashifu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Kuna maswali mengi sana kuhusiana na masuala mbalimbali, ipi nasaha yako kwa watafutaji elimu (wanafunzi) na wengineo kutokana na yaliojitokeza karibuni kuhusu video ya kashfa kwa Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم). Ipi nasaha zako kuhusiana na hilo?

 

 

JIBU:

 

 

Nasaha zetu kuhusiana na hilo ni kutulia na kuacha kukataza kwa njia hii; ya maandamano, au kushambulia wasiokuwa na hatia au kuharibu mali. Haya hayajuzu!

 

Lililo wajibu waliokuwa na jukumu la kujibu haya (maovu) ni Wanachuoni; si ‘awwaam (watu wasiokuwa na elimu). Wanachuoni ndio wanaojibu (na kukabiliana) mambo haya. Wao wanataka kutusumbua na kutuchokoza, Hili ndio lengo lao. Wanataka tupigane sisi kwa sisi. Askari wanazuia na hawa wengine wanashambulia. Hivyo inapelekea mapigano na mauwaji. Hili ndio lengo lao.

 

Tulieni! Tulieni! Waachieni jukumu Wanachuoni la kuwajibu watu hao. Au mtu kuachana nao kabisa.

 

Washirikina walikuwa wakimwambiaNabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) mchawi, kahini, muongo na mengineyo na Allaah Anamuamrisha kuwa na subira. Hakufanya maandamano Makkah. Hakubomoa chochote katika nyumba za washirikina. Hawakuua yeyote. Mtu asubiri na awe na utulivu mpaka hapo Allaah Atapowapatia Waislamu faraja.

 

Lililo wajibu ni mtu kutulia khaswa katika zama hizi na fitnah kama hizi na uovu huu wa sasa katika miji ya Waislamu. Ni wajibu kutulia na mtu kutokuwa na haraka (hamasa na jazba) katika mambo haya.

 

Na ‘awwaam (watu wa kawaida wasio na elimu) haiwastahiki kujiingiza katika hili. Wao hawajui mambo haya. Hakuna anayepaswa kushughulika na kujiingiza katika mambo haya isipokuwa tu Wanachuoni.

 

 

 

 

Share