071-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Jikinge Na Moto Japo Kwa Tende Au Neno Jema

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 71

 

Jikinge Na Moto Japo Kwa (Kutoa Swadaqa) Tende Au (Kutamka) Neno Jema

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ فَإِنْ لَمْ تَجِدْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ogopeni moto japo kwa (kutoa swadaqah) nusu tende, na usipopata basi kwa (kutamka) neno jema)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Kuogopa na kujikinga na moto kwa kila njia, ikiwa ni kutenda ‘amali kubwa au mno vipi kama mfano wa kutoa sadaka kokwa ya tende au neno jema, kwani moto wa Jahannam ni mkali mno! Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

  

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ﴿٦﴾

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu hawana huruma, shadidi, hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa. [At-Tahriym (66: 6)]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا ۚ لَّوْ كَانُوا يَفْقَهُونَ﴿٨١﴾

Sema: “Moto wa Jahannam ni mkali zaidi lau wangelifahamu.” [At-Tawbah (9: 81)]

 

 

 

2.  Yapendeza kutoa sadaka japokuwa kidogo mno na hakipotei chochote kinachotolewa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى), atakuja mja kukikuta katika hesabu yake Siku ya Qiyaamah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ  

Na mkopesheni Allaah karadhi nzuri. Na chochote kile cha kheri mnachokadimisha kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Allaah. Ni bora, na ujira mkubwa zaidi.  [Al-Muzzammil (73: 20)]

 

 

Rejea pia: Al-Baqarah (2: 110), (273), Aal-‘Imraan (3: 30),    At-Tawbah (9: 121).

 

 

 

3.   Neno jema ni sadaka anaposhindwa mtu kumpa sadaka muombaji, basi asimkaripie wala asimsimbulie kumfanyia maudhi bali ampe maneno mema. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى ۗ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ ﴿٢٦٣﴾

Kauli njema na msamaha ni bora kuliko swadaqah inayoifuata udhia. Na Allaah ni Mkwasi, Mvumilivu.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

264. Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri. [Al-Baqarah (2:263-264)]

 

Rejea pia: Adhw-Dhwuhaa (93: 10).

 

 

 

4.    Kutokudharau au kuacha kutenda jema lolote japo kama ni dogo mno vipi kwa sababu kila kitu kinaandikwa katika Daftari la matendo na mwana Aadam atakuja  kushuhudia kila jambo.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾

Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona.

 

وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona. [Al-Zalzalah (99: 7-8)]

 

 

Rejea pia Maryam (19: 76).

 

Na rejea Hadiyth namba (11).

 

 

 

5.    Neno jema linaunganisha nyoyo za Waumini na kujenga mapenzi.

 

Rejea: Aal-‘Imraan (3: 159), na linaweza kumuingiza kafiri katika Uislamu.

 

 

 

6.  Muumin daima ni mtendaji mema, kubwa na dogo, na haachi wala hachoki. Mfano wake ni kama mti mzuri utoao matunda mazuri kila mara kila wakati. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ ﴿٢٤﴾

Je, huoni vipi Allaah Amepiga mfano wa neno zuri kama mti mzuri mizizi yake imethibitika imara na matawi yake yanafika mbinguni? (marefu mno).

 

تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٥﴾

Unatoa mazao yake kila wakati kwa idhini ya Rabb wake. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu ili wapate kukumbuka.

 

وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ ﴿٢٦﴾

Na mfano wa neno baya ni kama mti mbaya uliong’olewa juu ya ardhi hauna imara. [Ibraahiym (14: 24-26)]

 

Na rejea Hadiyth namba (140) ambayo ni hitimisho ya Hadiyth iliyotoa mfano wa mti mzuri kumlinganisha na Muumini mwenye maneno mema.    

 

 

 

7. Fadhila za kutoa sadaka zimetajwa kwa wingi katika Qur-aan na Sunnah.

 

Rejea Hadiyth namba (31), (62), (77),

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share