086-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Atakayedhamini Ulimi Na Utupu Atadhaminiwa Jannah

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 86

 

Atakayedhamini Ulimi Na Utupu Atadhaminiwa Jannah

 

 

 

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ (رضي الله عنه) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ يَضْمَنْ لِي مَا بَيْنَ لَحْيَيْهِ وَمَا بَيْنَ رِجْلَيْهِ أَضْمَنْ لَهُ الْجَنَّةَ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa’d (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Atakayenidhaminia kilichomo baina ya taya zake (yaani ulimi) na kilichomo baina ya miguu yake (yaani utupu), nami nitamdhamini Jannah)).  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Hatari ya kutumia viungo viwili vya mwili katika maasi; ulimi na utupu ambavyo vinaweza kumpelekea mtu motoni.

 

Rejea Hadiyth namba (87), (88), (89), (93), (126).

 

 

2. Viungo viwili hivyo vinaweza kuwa ni sababu ya kufuzu au kuangamia mtu.

 

Rejea Al-Muuminuwn (23: 3) At-Twuur (52: 11-14).

 

 

3. Aayah kadhaa na Hadiyth kadhaa zimeonya kuhusu maovu ya ulimi kama vile kukufuru, kutukana, ghiybah, kuhamisha maneno, kufitinisha watu, ufedhuli n.k. Na adhabu zake ni duniani, kaburini na Aakhirah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾

Ole kwa kila mwenye kukebehi na kukashifu watu kwa ishara na vitendo na kwa kila mwenye kufedhehesha kwa ulimi. [Al-Humazah: 1]

 

Rejea pia Al-Hujuraat (49: 11-12), Al-Israa (17: 36)

 

 

 

4. Kila kiungo kitakuja kutamka maovu yaliyotendwa nacho hata ulimi pia utasema. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَوْمَ تَشْهَدُ عَلَيْهِمْ أَلْسِنَتُهُمْ وَأَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٤﴾

Siku zitakaposhuhudia dhidi yao ndimi zao, na mikono yao, na miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.  [An-Nuwr (24: 24)]

 

 

 

5-Rejea kisa cha ifk katika Al-Bukhaariy kilichoelezewa kirefu na mwenyewe ‘Aaishah (رضي الله عنها), na kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) katika An-Nuwr (24: 11-21), kisa ambacho ulimi ndio uliofanya kazi kumzulia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُم مَّا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ ۚ وَالَّذِي تَوَلَّىٰ كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١﴾

Hakika wale walioleta singizo la kashfa; (kumzulia ‘Aaishah  رضي الله عنها) ni kundi miongoni mwenu. Msiichukulie kuwa ni shari kwenu, bali ni kheri kwenu.  Kila mtu katika wao atapata yale aliyochuma katika dhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kuu.

 

لَّوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَـٰذَا إِفْكٌ مُّبِينٌ ﴿١٢﴾

Kwa nini mlipoisikia (kashfa ya kusingiziwa), Waumini wanaume na Waumini wanawake wasiwadhanie wenzao kheri, na wakasema: “Hii ni kashfa ya kusingizwa iliyo dhahiri?”

 

 

لَّوْلَا جَاءُوا عَلَيْهِ بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ ۚ فَإِذْ لَمْ يَأْتُوا بِالشُّهَدَاءِ فَأُولَـٰئِكَ عِندَ اللَّـهِ هُمُ الْكَاذِبُونَ ﴿١٣﴾

Kwa nini hawakuleta mashahidi wanne? Na kwa vile hawakuleta mashahidi, basi hao mbele ya Allaah ndio waongo.

 

 

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ لَمَسَّكُمْ فِي مَا أَفَضْتُمْ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٤﴾

Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na rahmah Yake duniani na Aakhirah, bila shaka ingekuguseni adhabu kuu kwa yale mliyojishughulisha nayo kuyaropoka,

 

 

إِذْ تَلَقَّوْنَهُ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُم مَّا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمٌ ﴿١٥﴾

Mlipoipokea (kashfa ya uzushi) kwa ndimi zenu, na mkasema kwa midomo yenu, yale ambayo hamkuwa na elimu nayo; na mnalidhania ni jambo jepesi; na hali hili mbele ya Allaah ni kubwa mno.

 

وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَا أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَـٰذَا سُبْحَانَكَ هَـٰذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ ﴿١٦﴾

Na kwa nini mlipoisikia (kashfa ya kusingiziwa) msiseme: “Haitupasi sisi tuzungumze haya; Subhaanak! Utakasifu ni Wako huu ni usingiziaji wa dhulma mkubwa mno!”

 

يَعِظُكُمُ اللَّـهُ أَن تَعُودُوا لِمِثْلِهِ أَبَدًا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧﴾

Allaah Anakuwaidhini msirudie abadani mfano wa haya, mkiwa ni Waumini wa kweli.

 

وَيُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٨﴾

Na Allaah Anakubainishieni Aayaat. Na Allaah Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٩﴾

Hakika wale wanaopenda uenee uchafu wa kashfa kwa wale walioamini; watapata adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.

 

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّـهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾

Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na rahmah Yake, na kwamba Allaah ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.

 

 

Na humo tunapata mafundisho kwamba pindi Muumini anaposikia usengenyaji au uzushi au usingiziaji wa kashfa anapaswa afanye yafuatayo:

 

  • Ajidhanie kheri na wema yeye mwenyewe kwanza, kwa hiyo asimdhanie nduguye maovu hayo.
  • Asiseme jambo au kudhania mpaka wapatikane mashahidi wanne.
  • Atambue kwamba ghiybah (kusengenya) na buhtaan (kusingizia uongo) si jambo dogo bali ni kubwa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى).  
  • Atambue kwamba usengenyeji na kumzulia mtu jambo ovu ni miongoni mwa dhulma ambayo itampatia khasara duniani na khasa Aakhirah.
  • Atanabahi kwamba haimpasi mtu kujisemea tu uzushi na usengenyaji, bali akimbilie kumtakasa  Allaah (سبحانه وتعالى) hapo hapo anaposikia kwa kusema “Subhaanak!”
  • Akhofu adhabu kali ya Allaah (سبحانه وتعالى) Aliyoahidi kuhusiana na maovu haya.
  • Atambue kwamba lau kama si fadhila za Allaah (سبحانه وتعالى) na Rahmah Zake basi ingewashika adhabu mapema zaidi na fedheha ya kusingizia jambo ambalo si la kweli, hivyo ingebalibakia kuwa ni majuto ya milele!

 

         

6. Hikma ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuvificha viungo viwili hivyo katika mwili wa bin Aadam kwa kuvihifadhi, na bin Aadam anapaswa naye kuvihifadhi kwa kutovitumia kwa maovu.

 

 

7. Tahadharisho la kutumia ulimi katika maovu, kwani ulimi juu ya kuwa ni kiungo kidogo, lakini ni mfalme wa viungo kama ilivyotajwa katika Hadiyth:  

 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، رَفَعَهُ قَالَ: ((إِذَا أَصْبَحَ ابْنُ آدَمَ فَإِنَّ الأَعْضَاءَ كُلَّهَا تُكَفِّرُ اللِّسَانَ فَتَقُولُ اتَّقِ اللَّهَ فِينَا فَإِنَّمَا نَحْنُ بِكَ فَإِنِ اسْتَقَمْتَ اسْتَقَمْنَا وَإِنِ اعْوَجَجْتَ اعْوَجَجْنَا))

 

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ((Anapoamka binaadamu, viungo vyote vinakufurisha [vinaonya maovu ya] ulimi: Mche Allaah kwa ajili yetu, kwani sisi tuko chini yako, ukinyooka nasi tunanyooka, na ukienda pogo, nasi tunapinda)). [At-Tirmidhiy, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (351), Swahiyh At-Tirmidhiy (2407)]

 

 

 

8. Muislamu akumbuke kwamba Malaika wawili wako tayari kuandika neno lolote linalotamkwa hata liwe dogo vipi. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ﴿١٦﴾

Na kwa yakini Tumemuumba insani na Tunajua yale yanayowaza nafsi yake, na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa koo.

 

إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ﴿١٧﴾

Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni. 

 

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾

Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf (50: 16-18)]

 

 

Rejea pia Al-Infitwaar (82: 10-12)].

 

 

9.  Neno moja tu litamkwalo likiwa zuri au ovu linaweza kuwa sababu ya kumridhisha au kumghadhibisha Allaah (سبحانه وتعالى) mpaka Siku ya Qiyaamah:

 

 

 عن أَبي عبد الرحمن بِلالِ بن الحارِثِ المُزَنِيِّ رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : ((إنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ رِضْوَانِ اللهِ تَعَالَى مَا كَانَ يَظُنُّ أنْ تَبْلُغَ مَا بَلَغَتْ يَكْتُبُ اللهُ لَهُ بِهَا رِضْوَانَهُ إِلَى يَومِ يَلْقَاهُ ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ سَخَطِ اللهِ مَا كَانَ يَظُنُّ أنْ تَبْلُغَ مَا بَلَغَتْ يَكْتُبُ الله لَهُ بِهَا سَخَطَهُ إِلَى يَوْمِ يَلْقَاهُ )). رواه مالك في المُوَطَّأ ، والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Abuu 'Abdir-Rahmaan Bilaal bin Al-Haarith Al-Muzniy (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Kwa hakika mja atazungumza neno linalomridhisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo Radhi Zake hadi Siku ya Qiyaamah. Na Kwa hakika mja atazungumza neno linalomkasirisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo hasira Zake hadi Siku ya Qiyaamah)) [Maalik katika Muwattwa na At-Tirmidhiy ambaye amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

 

 

10. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameonya kutokukaribia zinaa:

 

وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٣٢﴾

Na wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya kabisa.  [Al-Israa 17: 32)]

 

 

Rejea pia matahadharisho mengineyo ya kutokuzini na adhabu zake: An-Nuwr (24: 2), Al-Furqaan (25: 68).

 

 

11. Adhabu ya zinaa ni kali mno kwa jinsi kitendo hiki kilivyokuwa kiovu mno kwa sababu kinaathiri watendaje wake, na mtoto anayezaliwa kutokana na kitendo hicho cha zinaa, na huenda kikaathiri jamii nzima. Adhabu yake hiyo huenda ikastahiki kupigwa mawe mzinifu mpaka mauti yamfike kwa dalili ifuatayo:

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة وَزَيْد بْن خَالِد الْجُهَنِيّ فِي الْأَعْرَابِيَّيْنِ اللَّذَيْنِ أَتَيَا رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ أَحَدهمَا: يَا رَسُول اللَّه إِنَّ اِبْنِي هَذَا كَانَ عَسِيفًا - يَعْنِي أَجِيرًا - عَلَى هَذَا فَزَنَى بِامْرَأَتِهِ فَافْتَدَيْت اِبْنِي مِنْهُ بِمِائَةِ شَاة وَوَلِيدَة فَسَأَلْت أَهْل الْعِلْم فَأَخْبَرُونِي أَنَّ عَلَى اِبْنِي جَلْد مِائَة وَتَغْرِيب عَام وَأَنَّ عَلَى اِمْرَأَة هَذَا: الرَّجْم فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَأَقْضِيَنَّ بَيْنكُمَا بِكِتَابِ اللَّه تَعَالَى الْوَلِيدَة وَالْغَنَم رَدّ عَلَيْك وَعَلَى اِبْنك مِائَة جَلْدَة وَتَغْرِيب عَام. وَاغْدُ يَا أُنَيْس - لِرَجُلٍ مِنْ أَسْلَم - إِلَى اِمْرَأَة هَذَا فَإِنْ اِعْتَرَفَتْ فَارْجُمْهَا))  فَغَدَا عَلَيْهَا فَاعْتَرَفَتْ فَرَجَمَهَا - البخاري  و مسلم

 

kutoka kwa Abuu Hurayrah na Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy (رضي الله عنهما)  katika kisa cha Mabedui wawili waliokuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم),  mmoja alisema: "Ee Rasuli wa  Allaah, mwanangu (wa kiume) aliajiriwa na bwana huyu kisha akafanya zinaa na mke wake. Nimemlipa fidia kwa ajili ya mwanangu kwa kumpa kondoo mia moja na mtumwa mwanamke. Lakini nilipowauliza watu wenye elimu, wamesema kwamba mwanangu apigwe mijeledi mia na ahamishwe mji kwa muda wa mwaka na mke wa huyu bwana apigwe mawe hadi afariki".  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, nitahukumu baina yenu wawili kutokana na kitabu cha Allaah. Rudisha mtumwa mwanamke na kondoo na mwanao apigwe bakora mia kisha mwanao ahamishwe mbali kwa muda wa mwaka. Nenda Ee Unays!)) Alimwambia mtu katika kabila la Aslam, ((Nenda kwa mke wa huyu bwana na akikiri makosa yake, basi mpige mawe hadi mauti [yamfike])) Unays akamuendea na akakiri makosa yake, kwa hiyo akampiga mawe hadi mauti. [Al-Bukhaariy na Muslim]

  

Share