Mke Hataki Kujifunza Dini Ya Kiislam Na Hana Mapenzi Na Mume

 

SWALI:

mke wangu hataki nimfunze  dini kila nikimwabia anasema hana wakati, hawezi kuvaa hijaab eti angaliki mtoto mdogo, mapenzi hana kwangu, nikimtaka kwa kitendo cha ndowa anadai amecoka, mara anasema eti hataki anakazi za nyumabani yaani hataki kujuwa kitu chochote cha islam pia hanitoshelezi kimapenzi hana mapokezi mazuri kwangu mapishi na kadhalika siwezi kuyamaliza mabo yote ni mengi sana yaani kwa kifupi sina raha ya mke wangu hata kidogo na inajuzu kukerahika hivi?na nikiondoka duniani katika hali iyi itakuwa vipi?

Nimeamuwa kumuacha lakini nimesema niulize kwanza wanacuoni kabla ya kucujuwa hatuwa yoyote yaani nilfanya subira huwu ni mwaka wa tatu sasa nasubiri. Najuwa kama ina laha maswabirina nafsi yangu imecoka mungu mweney anaona. Nakavyo ona ni aduwi wa kiislam ndio mana nataka niepukane nae sasa ni ipi njiya nzuri ya kuepukana nae kwa kisheria?

na hajuwi mabo ya ku kaa eda wala talaka nitafanyaje?

Nasubiri jibu lenu na najuwa kama mnakazi nyingi mno kwa matarajio ya kupata jibu langu haraka iwezekanvyo inshaallah wasalam alaikum warahamtulahi wa barakatu.

 


 

 

 

JIBU:

AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hili ni tatizo letu kubwa katika jamii yetu ya kuoa au kuolewa kwa sababu ya uzuri, mali, jaha na nasaha lakini kisha majuto yanakuwa makubwa

sana juu yetu. Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuusia kuwa tuoane kwa sababu ya Dini na maadili lakini sisi tunasema la hivyo sivyo na haya ndiyo yanakuwa matokeo.

Hivyo, tunatakiwa kubadili mienendo yetu ili yaende sambamba na Sunnah za Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na huu usumbufu utakuwa ni wenye kuondoka katika jamii.

Nasaha zetu katika hilo tatizo ni kukuambia kuwa ujipatie muda wa kuweza kumnasihi tena pamoja na kumpatia mawaidha ili arudi katika Dini pamoja na kutekeleza wajibu wake katika nyumba yenu. Ikiwa baada ya huo muda hajajirekebisha basi chukua hatua ya pili nayo ni kumhama katika malazi hadi atakapojirudi.

Ikiwa hata kwa hilo hakuwa ni mwenye kurudi katika njia ya sawa basi ikiwa wapo Mashaykh ambao wanaweza kutoa ushauri nasaha katika hiyo sehemu unayoishi unaweza kuwatumia ili watatue tatizo hilo.

Ikiwa imeshindikana basi chukua hatua ya mwisho nayo ni kufanya kikao baina yako wewe, mkeo, na jamaa wa karibu (maana kama wazazi wake si Waislam huenda ikawa vigumu wao kuingilia) na ikiwa nia ni kutaka suluhu basi itapatikana. Ikiwa hakuna matokeo mazuri katika kikao hicho basi ni afadhali muachane, huenda yeye akapata mume atakayemridhi kwa tabia zake hizo na wewe kutunukiwa yule ambaye atakwenda sambamba na matarajio yako. Na ukifanya hivyo kwa sababu ya kulinda Dini yako, Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hatakuacha bali Atakupa badali nzuri. Na ikifikia hali hiyo, tunakushauri sana utafute mwanamke wa Kiislam na ambaye anafuata dini yake vizuri na mwenye tabia njema.

Kuhusu talaka na eda si mambo mazito kwani unaweza ukamfundisha yanayotakiwa kufanywa na yeye katika kipindi hicho. Baada ya hapo ni yeye mwenyewe kutekeleza hayo ambayo yanafaa kutekelezwa.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share