Imaam Ibn Rajab - Kunasibishwa Mwezi Wa Muharram Na Allaah

 

Kunasibishwa Mwezi Wa Muharram Na Allaah 

 

Ibn Rajab (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

Imaam Ibn Rajab (Rahimahu-Allaah) amesema:

 

"Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameuita mwezi Muharram kuwa ni Mwezi wa Allaah na kuunasibisha kwa Allaah inaashiria utukufu na fadhila zake kwani Allaah hunasibisha kwake kile ambacho ni makhsusi miongoni mwa viumbe Vyake, mfano; Alivyomnasabisha Muhammad, Ibraahiym, Is-haaq, Ya’-quwb na wengineo miongoni mwa Manabii - kuwahusisha na 'ubuwdiyyah Yake. (Yaani  Amemwita Muhammad: “Mja Wake” [Suwrat Al-Israa: 1, An-Najm: 10],  Akawataja hao wengine kama ni: “Waja Wangu” [Suwrat Swaad: 45]) Akajinasibisha na Nyumba Yake (Yaani Al-Ka’bah kwa kusema “Nyumba Yangu” [Al-Baqarah: 125]) Na ngamia Wake wa kike (Yaani kusema: “Ngamia wa kike wa Allaah” [Suwrat Al-A’raaf: 73, Suwrat Ash-Shams: 13])

 

 

[Latwaaif Al-Ma’aarif, uk. 36]

 

Share