004-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AR-RAHMAAN

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

الرَّحْمن

004 - AR-RAHMAAN

 

 

 

AR-RAHMAAN: Mwingi wa rahmah:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

الرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾ عَلَّمَ الْقُرْآنَ ﴿٢﴾

Ar-Rahmaan; Mwingi wa rahmah. Amefundisha Qur-aan [Ar-Rahmaan: 1-2]

 

Jina hili ni pana zaidi na lenye kuenea zaidi kuliko Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu). Hili linakusanya maana zote za rahmah, huruma n.k. Allaah Ndiye Mwenye rahmah iliyokusanya kila kitu, iliyoenea kwa viumbe Vyake vyote duniani, bin Aadam kwa majini, Waumini kwa makafiri, wanyama, mimea, hakuna yeyote au chochote katika kuwepo kwake ila rahmah Yake imemuenea, na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema: 

 

الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾

Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah), Ar-Rahmaan; Mwingi wa Rahmah, basi ulizia kuhusu Yeye, (kwani Yeye) ni Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana. [Al-Furqaan: 59]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan; Mwingi wa Rahmah juu ya ‘Arshi Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah) [Twaahaa 5]

 

Istawaa katika ‘Arshi kwa jina la Ar-Rahmaan, kwa sababu ‘Arshi imezungukwa na viumbe na ina wasaa kwao, na rahmah imewazunguka waja Wake, ina wasaa kwao kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ

Na rahmah Yangu imeenea kila kitu [Al-A’raaf: 156]

 

Istawaa katika kilicho kipana zaidi katika Alivyoviumba, nayo ni ‘Arsh Yake na kwa sifa iliyo pana zaidi nayo ni rahmah Yake. Na kwa ajili hiyo rahmah Yake imeenea katika kila kitu.

 

Ar-Rahmaan ni jina Analoitwa Allaah Peke Yake. Ama athari ya jina hili ni kwa wote; kwa watu wema na waovu. Na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amelitaja zaidi Jina hili katika Suwrah ziloteremshwa Makkah, khasa katika Suwrat Maryam ambayo imetajwa mara  nyingi zaidi ya Suwrah nyinginezo.

 

Kipindi hicho cha Makkah ni kipindi cha mwanzo cha Uislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawadhihirishia makafiri Sifa Yake hiyo kwamba Yeye ni Mwingi wa rahmah juu ya kuwa wanamshirikisha.

 

Na katika Sunnah zimethibiti Hadiyth kadhaa kuhusu rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wanayorehemeana viumbe ardhini:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((إِنَّ اللَّهَ خَلَقَ الرَّحْمَةَ يَوْمَ خَلَقَهَا مِائَةَ رَحْمَةٍ، فَأَمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعًا وَتِسْعِينَ رَحْمَةً، وَأَرْسَلَ فِي خَلْقِهِ كُلِّهِمْ رَحْمَةً وَاحِدَةً، فَلَوْ يَعْلَمُ الْكَافِرُ بِكُلِّ الَّذِي عِنْدَ اللَّهِ مِنَ الرَّحْمَةِ لَمْ يَيْأَسْ مِنَ الْجَنَّةِ، وَلَوْ يَعْلَمُ الْمُؤْمِنُ بِكُلِّ الَّذِي عِنْدَ اللَّهِ مِنَ الْعَذَابِ لَمْ يَأْمَنْ مِنَ النَّارِ)) البخاري في الأدب، باب جعل الله الرحمة في مائة جزء  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika Allaah Ameumba rahmah. Siku Aliyoumba Alizifanya rahmah mia (100) Akazuia Kwake rahmah tisini na tisa (99) Akateremsha rahmah moja kwa viumbe Vyake vyote.  Lau kafiri angelijua kuhusu rahmah zilizokuweko kwa Allaah, basi asingekata tamaa kuingia Jannah. Na lau Muumini angejua adhabu zilizoko kwa Allaah, basi asingejiaminisha na moto)) [Al-Bukhaariy fiy Ar-Riqaab Baab Ar-Rajaa ma’al-khawf]

 

وعن أبي هريرة رضي الله عنه أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((جَعَلَ الله الرَّحْمَةَ مِائَةَ جُزْءٍ، فَأَمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ جُزْءًا وَأَنْزَلَ فِي الأَرْضِ جُزْءًا وَاحِدًا، فَمِنْ ذَلِكَ الْجُزْءِ يَتَرَاحَمُ الْخَلْقُ حَتَّى تَرْفَعَ الْفَرَسُ حَافِرَهَا عَنْ وَلَدِهَا خَشْيَةَ أَنْ تُصِيبَهُ)) البخاري في الأدب، باب جعل الله الرحمة في مائة جزء   

Na pia amepokea Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Amejaalia rahmah mia, Akazuia Kwake rahmah tisini na tisa, Akateremsha moja tu ardhini. Basi kutokana na hiyo ndio wanayorehemeana viumbe hadi kwamba farasi huinua makwato yake kukhofia asimkanyage mtoto wake)) [Al-Bukhaariy Baab Ja’ala Allaahu Ar-Rahmah fiy miat juz’]

 

 عَنْ عَطَاءٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ لِلَّهِ مِائَةَ رَحْمَةٍ أَنْزَلَ مِنْهَا رَحْمَةً وَاحِدَةً بَيْنَ الْجِنِّ وَالإِنْسِ وَالْبَهَائِمِ وَالْهَوَامِّ فَبِهَا يَتَعَاطَفُونَ وَبِهَا يَتَرَاحَمُونَ وَبِهَا تَعْطِفُ الْوَحْشُ عَلَى وَلَدِهَا وَأَخَّرَ اللَّهُ تِسْعًا وَتِسْعِينَ رَحْمَةً يَرْحَمُ بِهَا عِبَادَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ))     

Na pia imepokelewa kutoka kwa ‘Atwaa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ana rahmah mia, Ameiteresha moja kati ya majini na wana Aadam na wanyama na wadudu, ambao wanaoneana huruma na wanarehemeana, na hiyo hiyo mpaka mnyama mwitu anamhurumia mwanawe. Akazuia Allaah rahmah tisini na tisa Atawarehemu kwazo waja Wake Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (6/98), Ahmad (2/434), Ibn Maajah (4293)]

 

Sifa hii ya Rahmah ni ya dhati Yake Allaah ambayo haiwezi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Makafiri wa Makkah hawakupenda Jina hili la Ar-Rahmaan wakakataa kuliandika katika mkataba wa Hudaybiyah pale Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomuamrisha mwandishi wa mkataba andike “BismiLLaah (Kwa Jina la Allaah) Ar-Rahmaan (Mwingi wa rahmah) Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu).” Wakasema: “Andika: Biismika-Allaahumma.”

Hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akateremsha:

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ  

Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan; Mwingi wa rahmah, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa.   [Al-Israa: 110]

[Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Na ndio maana Suwrah za Qur-aan zinaanza na BismiLLaah inayotaja Majina Yake Mawili ya Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym, na pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametanguliza katika ufunguzi wa Suwrat Al-Faatihah Akaanza na Ar-Rahmaan (Mwingi wa rahmah) na Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu).

 

Vipi Uweze kupata rahmah ya Allaah?

 

1. Njia ya kwanza kuweza kupata Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni yale yote yenye uhusiano wa mtu na Rabb Wake kama vile:  

 

Kujipuesha na yote yaliyoharamishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu baadhi ya yaliyoharamishwa yanamsababisha mtu kupata laana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) inayomaanisha ni kuwekwa mbali na rahmah Zake.   

Pia katika njia ya kupata rahmah ya Allaah, ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾

Na mtiini Allaah na Rasuli mpate kurehemewa.  [Aal-‘Imraan: 132]

 

Na pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametaja sifa za waja Wake ambao amehusisha na Jina na Sifa Yake hii ya Ar-Rahmaan Anawaita: ‘Ibaadur-Rahmaan (Waja wa Rahmaan).” Pindi atakapotekeleza mtu hayo yaliyotajwa katika Suwratul-Furqaan Aayah 63 mpaka Aayah 76 basi atastahiki kuwa ni miongoni mwa ‘Ibaadur-Rahmaan.

 

وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾

Na waja wa Ar-Rahmaan Mwingi wa Rahmah ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam!

 

وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾

Na wale wanaokesha (baadhi ya) usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama…..  [Al-Furqaan: 63-76]

 

Hali kadhaalika kuzidisha ‘ibaadah kwa wingi, Swalaah za usiku (tahajjud), kuomba du’aa, kuisikiliza kwa makini na kuisoma Qur-aan, kuzingatia maana zake, kuwa na taqwa, kusimamisha Swalaah na kutoa Zakaah, kufanya jihaad katika njia ya Allaah, kuvuta subira katika mitihani na misiba, kuomba maghfirah, na kwa ujumla ni kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

“Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako.” (Allaah) Akasema: “Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (na hoja, dalili) Zetu.” [Al-A’raaf: 156]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Aayah zifuatazo:

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٥٦﴾

Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Rasuli ili mpate kurehemewa. [An-Nuwr: 56]

 

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾

Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [Al-A’raaf: 204]

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٥٥﴾

Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe na taqwa mpate kurehemewa. [Al-An’aam: 155]

 

 

قَالَ يَا قَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ ۖ لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٦﴾

(Swaalih) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnahimiza uovu kabla ya mema; kwa nini msimwombe Allaah maghfirah huenda mkarehemewa?” [An-Naml:  46]

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.

 

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿١٥٦﴾

Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”

 

أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

Hao zitakuwa juu yao barakah kutoka kwa Rabb wao na rahmah, na hao ndio wenye kuongoka. [Al-Baqarah: 155-157]

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾

Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana jihaad katika njia ya Allaah, hao wanataraji rahmah ya Allaah, na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Baqarah:  218]

 

Na kuomba du’aa ni ambazo zimethibiti katika Sunnah za kumwomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) rahmah Yake mifano ya du’aa mbili miongoni mwa du’aa nyingi ni:

 

اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت

 

Allaahumma Rahmatika arjuw falaa takilniy ilaa nafsiy twarfata ‘aynin, wa aswlih liy sha-aniy kullahu, laa ilaaha illaa Anta

 

Ee Allaah, nataraji rahmah Zako, usinitegemeze  kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, na Unitengenezee mambo yangu yote, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe [Hadiyth ya Abu Bakr Nafiy’ bin Haarith Ath-Thaqafiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) - Abu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42),  ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy  katika Swahiyh Abi Daawuwd (3/959) ]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مُوجِبَاتِ رَحْمَتِكَ، وَعَزَائِمَ مَغْفِرَتِكَ، وَالسَّلامَةَ مِنْ كُلِّ إِثْمٍ، وَالْغَنِيمَةَ مِنْ كُلِّ بِرّ، وَالْفَوْزَ بِالْجَنَّةِ، وَالنَّجَاةَ مِنَ النَّاَرِ.

Allaahumma inniy as-aluka muwjibaati Rahmatik wa 'azaaim maghfiratik was-salaamata min kulli ithm, wal ghaniymata minkulli birr, wal fawza bil Jannati, wan najaata minan-naari

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba azima za rahmah Yako, azimio la maghfirah Yako, na amani katika kila dhambi, na ghanima katika kila jema, na kufuzu katika Jannah na kuokoka na moto [Al-Haakim (1/525) na ameipa daraja ya Swahiyh na ameiwafiki  Adh-Dhahabiy]

 

 

2. Njia ya pili ya kuweza kupata Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  ni yale yote yenye uhusiano wa bin Aadam na viumbe vinginevyo.

 

Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah) amesema: “Rahmah ya mja kwa viumbe ni sababu kuu inayomfikisha mtu kupata rahmah ya Allaah ambayo taathira yake ni kupata khayraat za dunia na khayraat za Aakhirah, na kukosa kwake ni kukatwa na kuzuilika kupata rahmah ya Allaah. Na mja anahitaji kwa dharura rahmah ya Allaah, asiikose hata kidogo kadiri ya muda wa upepeso wa jicho. Na kila kilichopo chenye neema na kukimbiza balaa, ni katika rahmah ya Allaah.

 

Basi anapotaka kubakia katika rahmah ya Allaah na kuzidi kuipata na afanye yote yanayosababisha kupata rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Yote yanajumuika katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾

Hakika rahmah ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan. [Al-A’raaf: 56]

[Bahjatu Quluwb Al-Abraar, uk. 197-198]

 

Hadiyth nyingi za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zimethibiti kuhusu kupata rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kufanya ihsaan na wema. Baadhi ya Hadiyth ni kama zifuatazo:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو يَبْلُغُ بِهِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الرَّاحِمُونَ يَرْحَمُهُمْ الرَّحْمَنُ ارْحَمُوا مَنْ فِي الْأَرْضِ يَرْحَمْكُمْ مَنْ فِي السَّمَاءِ

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr  kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema: ((Ar-Rahmaan Atawarehemu wenye kurehemu. Mrehemuni aliyeko ardhini Atakurehemuni Aliyeko mbinguni)) [Sunan At-Tirmidhiy (1924) Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy, Swahiyh Abiy Daawuwd (4941), Swahiyh At-Targhiyb (2256)]

 

قال رسول الله - صلى الله عليه وسلّم: ((مَنْ لاَ يَرْحَمِ النَّاسَ لاَ يَرْحَمْهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ‏)) رواه البخاري (6013) ومسلم (2319)

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Asiyerehemu watu hatorehemewa na Allaah Aliyetukuka na Aliye Jalali)) [Al-Bukhaariy (6013) Muslim (2319)]

 

Kusulihisha waliokhasimikiana:

 

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٠﴾

Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa. [Al-Hujuraat: 10]

 

Na Sifa hii ya rahmah imehusiana na Ar-Rahm (fuko la uzazi) ambalo kwalo ndugu na jamaa hurehemeana na likawa jambo la kukata undugu ni dhambi kubwa mno inayosababisha laana za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na ghadhabu Zake kama ilivyotajwa katika Qur-aan. [Muhammad: 47: 22-23] Na pia Akasisitiza mno katika Qur-aan [Al-Baqarah: 27, Ar-Ra’d: 20-21]. Na pia Hadiyth kadhaa zimethibiti makemeo na khatari ya kukata undugu hadi kwamba inamharamisha Muislamu kuingia Jannah. Na katika Hadiyth zifuatazo zimehusisha sifa hiyo ya rahmah na undugu:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: ((إِنَّ الرَّحِمَ شَجْنَةٌ مِنْ الرَّحْمَنِ، فَقَالَ اللَّهُ: مَنْ وَصَلَكِ وَصَلْتُهُ وَمَنْ قَطَعَكِ قَطَعْتُهُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Ar-Rahm [fuko la uzazi]  linatokana na Jina la Ar-Rahmaan; Basi Allaah Amesema: Atakayekuunga Nami Nitamuunga na Atakayekukata Nami Nitamkata)) [Al-Bukhaariy 5988]

 

Na pia:

عنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ، تَقُولُ مَنْ وَصَلَنِي وَصَلَهُ اللَّهُ وَمَنْ قَطَعَنِي قَطَعَهُ اللَّهُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ar-Rahm [fuko la uzazi] limetundikwa katika ‘Arshi, linasema: Anayeniunga Allaah Atamuunga, na anayenikata Allaah Atamkata)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na katika kuwarehemu wanyama:

 

Mwanamke kahaba aliyemnywesha mbwa maji alighufuriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ غُفِرَ لِامْرَأَةٍ مُومِسَةٍ مَرَّتْ بِكَلْبٍ عَلَى رَأْسِ رَكِيٍّ يَلْهَثُ قَالَ كَادَ يَقْتُلُهُ الْعَطَشُ فَنَزَعَتْ خُفَّهَا فَأَوْثَقَتْهُ بِخِمَارِهَا فَنَزَعَتْ لَهُ مِنْ الْمَاءِ فَغُفِرَ لَهَا بِذَلِكَ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ameghufuriwa mwanamke kahaba. Alimpitia mbwa akihaha (kwa kiu) karibu na kisima. Alipoona anakaribia kufa kwa kiu, alivua kiatu chake akakifunga kwenye shungi lake akamchotea maji. Allaah Akamghufuria kwa kufanya hivyo)) [Al-Bukhaariy (3143) Muslim (2245)]

 

Mwanamke aliyemuadhibu paka aliingizwa motoni:

 

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((عُذِّبَتْ امْرَأَةٌ فِي هِرَّةٍ حَبَسَتْهَا حَتَّى مَاتَتْ جُوعًا فَدَخَلَتْ فِيهَا النَّارَ, لاَ هِيَ أَطْعَمْتِهَا  وَسَقَيْتِهَا إِذْ هِيَ حَبَسْتِيهَا وَلاَهِيَ تَرَكَتْها تَأكُلُ مِنْ  خَشَاشِ الأرْضِ)) متفق

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwanamke fulani aliadhibiwa kwa sababu ya paka aliyemfungia mpaka akafa kwa njaa, akaingia motoni [kwa sababu] alipomfungia hakumpa chakula wala hakumnywesha maji wala hakumwacha aende akale vidudu ardhini. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share