011-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: ADHW-DHWAAHIRU

 

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

الظَّاهِرُ

ADHW-DHWAAHIRU

 

 

Adhw-Dhwaahiru: Aliye juu kabisa hakuna kitu juu Yake.

 

Imetajwa katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾

Yeye Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yake, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yake, na Aliye juu kabisa hakuna kitu juu Yake, na Aliye karibu kabisa, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.  [Al-Hadiyd: 3]

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

  وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَليْسَ فَوْقَكَ شيء،  

…Nawe Uko juu kabisa hakuna kitu juu yako… [Muslim]

 

Yeye ni Dhahiri kwa vitendo Vyake na hukusudiwa kwa maana nyinginezo mfano: kuwa juu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

فَمَا اسْطَاعُوا أَن يَظْهَرُوهُ

Basi (Ya-juwj na Ma-juwj) hawakuweza kuukwea. [Al-Kahf: 97]

 

yaani kupanda juu yake. Pia ina maana ya kushinda, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ ﴿١٤﴾

Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi. [Asw-Swaff: 14]

 

Pia ina maana kusaidia na kama ilivyothibiti katika Suwrat At-Tahriym Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ﴿٤﴾

Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia. [At-Tahriym: 4]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩﴾

Hakika Allaah Anakukatazeni tu kuhusu wale waliokupigeni vita katika Dini, na wakakutoeni kutoka majumbani mwenu, na wakasaidiana juu ya kukutoeni. [Al-Mumtahinah: 9]

 

yaani: wakawasaidia, au kudhihirisha kilichojificha.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Adhw-Dhwaahir:

 

1. Kila kitu kipo chini Yake, na Yeye yupo juu ya kila kitu, hakuna kilichokuwa juu yake [Ibn Jariyr (11/670)]

 

i-       Ujuu wa dhati,

ii-     Na ujuu wa ushindi,

iii-   Ujuu wa shani na uwezo na sifa ya ukamilifu.

 

2. Yeye (‘Azza wa Jalla) ni Adhw-Dhwaahir kwa dalili mbali mbali, kwa Aayah na kwa hoja madhubuti zenye kuthibitisha kupwekeka kwake.

 

3. Yeye (‘Azza wa Jalla) ni Adhw-Dhwaahir Ndiye Ambaye humuona na kumdhihirishia kila Amtakaye katika waja Wake, katika elimu na sayansi mbali mbali, na maarifa ya kiakili na ya kunukuu na ya ghayb. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٣﴾

Na pale Nabiy alipompa mmoja wa wake zake jambo la siri, na huyo mke alipoipasha habari na Allaah Akamdhihirishia (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم), akataarifu baadhi yake na akaacha nyingine [At-Tahriym: 3]

 

Na Anasema (‘Azza wa Jalla):

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا ﴿٢٦﴾

Mjuzi wa ghayb na wala Hamdhihirishii yeyote ghayb Yake.

 

إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا ﴿٢٧﴾

Isipokuwa yule Aliyemridhia miongoni mwa Rasuli basi hakika Yeye Anamwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.  [Al-Jinn: 26-27]

 

4. Naye ni Adhw-Dhwaahir Ambaye Ametukuza Dini hii pamoja na wenye Dini hii juu ya kila dini, na Akajaalia ni yenye kushinda katika hoja, katika upanga, kwa watu wote, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [At-Tawbah: 33]

 

5. Naye (‘Azza wa Jalla) ni Adhw-Dhwaahir Mwenye kuwasaidia waja Wake wote, katika kupata riziki zao, katika maisha yao, katika kuwepesisha mambo yao, na katika manufaa ya dunia yao, na mengine maalum kwa vipenzi Vyake wenye kumpwekesha. Hao Anawaneemesha katika mambo ya dunia yao, katika marejeo yao, kuwanusuru na adui zao, na kuwazuilia na vitimbi vyao, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ ﴿١٤﴾

Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi. [Asw-Swaff: 14]

 

Kwa hakika kufanya ‘ibaadah kwa kumuomba du’aa kwa Jina Lake (‘Azza wa Jalla), Adhw-Dhwaahir hukusanya moyo wa mja kwa Rabb wake, na kumfanya Ndiye Rabb Anayekusudiwa katika haja zake zote na marejeo yake ya kila kitu.  Jambo hilo likitulia kwa mja na kujua kuwa Rabb wake Ndiye haswa Adhw-Dwaahir basi uja wake utanyooka na kurejea Kwake katika kila hali na kila wakati.

 

 

 

Share