05-Kitaab At-Tawhiyd: Wito Wa Kushuhudia Kwamba Laa Ilaaha Illa-Allaah

Mlango Wa 5

بَابُ اَلدُّعَاءِ إِلَى شَهَادَةِ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ

Wito Wa Kushuhudia Kwamba Laa Ilaaha Illa-Allaah


 

وَقَوْلِهِ تَعَالَى:

Na kauli Yake Ta’aalaa:

 

 قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٨﴾

((Sema: “Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah, juu ya nuru za elimu na umaizi, mimi na anayenifuata. Na Subhaana-Allaah! Utakasifu ni wa Allaah, nami si miongoni mwa washirikina.”)) [Yuwsuf (12:108)]

 

 وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  لَمَّا بَعَثَ مُعَاذًا إِلَى الْيَمَنِ: قَالَ لَهُ: ((إِنَّكَ تَأْتِي قَوْمًا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ، فَلْيَكُنْ أَوَّلَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ شَهَادَةَ أَن لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ)) وَفِي رِوَايَةٍ: ((إِلَى أَنْ يُوَحِّدُوا اَللَّهَ. فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوكَ لِذَلِك فَأَعْلِمْهُمْ أَنَّ اَللَّهَ اِفْتَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ. فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوكَ لِذَلِكَ فَأَعْلِمْهُمْ أَنَّ اَللَّهَ اِفْتَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ فَتَرُدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ. فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوكَ لِذَلِكَ فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ, وَاتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ فَإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ اَللَّهِ حِجَابٌ)) أَخْرَجَاهُ

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtuma Mu’aadh Yemen alimwambia: ((Hakika wewe utakutana na watu miongoni mwa Ahlul-Kitaab, basi jambo la kwanza la kuwalingania liwe ni kushuhudia kwamba: Laa ilaaha illa-Allaah- hapana Muabudiwa wa haki kuabudiwa ila Allaah)) Na katika riwaayah nyingine: (([Walinganie] Kumpwekesha Allaah. Watakapokutii hilo, wajulishe kwamba Allaah Amewafaradhishia Swalaah tano usiku na mchana. Watakapokutii hilo, basi wajuilshe kwamba Allaah Amewafaradhishia Zakaah iichukuliwe kutoka kwa matajiri wao na kupewa masikini wao. Watakapotii hilo, basi tahadhari kuchukua bora za mali zao [kama malipo ya Zakaah], na tahadhari na du’aa ya aliyedhulumiwa, kwani hakuna kizuizi baina yake na Allaah)) [Al-Bukhaariy (1395) Muslim (19)]

 

وَلَهُمَا عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ يَوْمَ خَيْبَر: ((لاُعْطِيَنَّ اَلرَّايَةَ غَدًا رَجُلاً يُحِبُّ اَللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيُحِبُّهُ اَللَّهُ وَرَسُولُهُ, يَفْتَحُ اَللَّهُ عَلَى يَدَيْهِ)) فَبَاتَ اَلنَّاسُ يَدُوكُونَ لَيْلَتَهُمْ، أَيُّهُمْ يُعْطَاهَا، فَلَمَّا أَصْبَحُوا غَدَوْا عَلَى رَسُولِ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) كُلُّهُمْ يَرْجُو أَنْ يُعْطَاهَا فَقَالَ:((أَيْنَ عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ؟)) فَقِيلَ هُوَ يَشْتَكِي عَيْنَيْهِ. فَأَرْسَلُوا إِلَيْهِ، فَأُتِيَ بِهِ فَبَصَقَ فِي عَيْنَيْهِ، وَدَعَا لَهُ فَبَرَأَ كَأَنْ لَمْ يَكُنْ بِهِ وَجَعٌ، فَأَعْطَاهُ اَلرَّايَةَ، فَقَالَ: ((اُنْفُذْ عَلَى رِسْلِكَ، حَتَّى تَنْزِلَ بِسَاحَتِهِمْ، ثُمَّ اُدْعُهُمْ إِلَى الإِسْلامِ, وَأَخْبِرْهُمْ بِمَا يَجِبُ عَلَيْهِمْ مِنْ حَقِّ اَللَّهِ تَعَالَى فِيهِ، فَوَاَللَّهِ لأَنْ يَهْدِيَ اَللَّهُ بِكَ رَجُلاً وَاحِدًا خَيْرٌ لَكَ مِنْ حُمْرِ اَلنَّعَمِ))  يَدُوكُونَ أَيْ يَخُوضُونَ

Na kutoka kwao wawili pia: Imepokelewa toka kwa Sahl bin Sa’d (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema siku ya Khaybar: ((Kesho nitamkabidhi bendera mtu anayempenda Allaah na Rasuli Wake na Allaah na Rasuli Wake wanampenda. Allaah Atampa ushindi mikononi mwake)). Watu wakakesha usiku wakishughulika kujadili nani atakayepewa bendera. Asubuhi walimwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hamu wakitegemea kupewa bendera. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akauliza: ((Yuko wapi ‘Aliy bin Abiy Twaalib?)). Wakajibu: Anauguwa macho yake mawili. Akaagizwa akafika. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatema mate machoni mwake kisha akamwombea akapona kana kwamba hakuwa na maumivu yoyote. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akampa bendera akamwambia: ((Waendee kwa taratibu na upole mpaka ufikie katikati yao, kisha waite katika Uislamu na wajulishe wajibu wao katika haki ya Allaah. Naapa kwa Allaah! Allaah Akimuongoa mtu mmoja katika Uislamu kupitia kwako, basi ni khayr kuliko ngamia wekundu)) [Al-Bukhaariy (2942) Muslim (2406)]

 

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kulingania kwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni miongoni mwa njia za kumfuata Rasuli wa Allaah.

 

2-Msisitizo juu ya ikhlaasw kwa kuwa watu wengi wajidai kulingania katika haki lakini ni kwa ajili ya maslahi ya nafsi zao.

 

3-Kulingania kwa ‘Baswiyraa’ (busara, utambuzi, umaizi na ujuzi wa Dini yetu) ni faradhi mojawapo.

 

4-Miongoni mwa dalili za uzuri wa Tawhiyd ni kumtakasa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumwepusha Allaah (سبحانه وتعالى) na kila aibu na kasoro. 

 

5-Miongoni mwa maovu ya shirki ni kumtukana Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumnasibisha na yasiyomstahiki.

 

6-La muhimu kabisa ni Muislamu kujiweka mbali na watu wa shirki hata kama hafanyi shirki wakati anapokuwa pamoja nao.

 

7-Tawhiyd (na kuilingania) ni wajibu wa kwanza kabisa kwa Muislamu.

 

8-Tawhiyd iko mbele ya kila kitu, hata Swalaah.

 

9-Maana ya “wampwekeshe Allaah” katika ‘ibaadah ni sawa na maana ya kushuhudia Laa ilaaha illaa Allaah.

 

10-Ingawa mtu anaweza kuwa katika Ahlul-Kitaab na asijue maana ya Tawhiyd au kuitekeleza. Au anaweza kuwa anajua, lakini matendo yake yakawa kinyume.

 

11-Msisitizo wa kufundisha kwa utaratibu maalumu; jambo moja baada ya jingine.

 

12-Kuanza kufundisha mambo muhimu zaidi kisha linalofuatia kwa umuhimu.

 

13-Ugawaji wa Zakaah.

 

14-Mwenye elimu amuondolee mashaka mwanafunzi.

 

15-Wakusanyaji wa Zakaah wazuiwe wasichukue mali zilizo bora kabisa za watu.    

 

16-Kuogopa du’aa ya aliyedhulumiwa.

 

17-Maelezo kuwa du’aa ya aliyedhulumiwa haina kizuizi baina yake na Allaah (سبحانه وتعالى).

 

18-Miongoni mwa dalili za Tawhiyd ni kuwa, Rasuli na awliyaa wa mwanzo kabisa walipata tabu, mateso, njaa na maradhi.

 

19-Kauli yake, ((nitampa bendera …)) ni alama ya Unabiy.

 

20-Kumtemea mate ‘Aliy(رضي الله عنه)  machoni mwake akapona, pia ni alama ya Unabiy.

 

21-Fadhila za ‘Aliy (رضي الله عنه).

 

22-Fadhila za Maswahaba kuwa walikesha usiku wakiwazia (nani atakayepewa bendera) na kisha kushughulishwa kwao na bishara ya ushindi wa mji.

 

23-Ukumbusho kuhusu kuamini Al-Qadar; kwa kuwa hiyo (yaani bendera) alipewa mtu ambaye hakuitaraji au kuiomba, na wakanyimwa walioitaraji.

 

24-Adabu katika kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ((Waendee kwa taratibu na upole…)).

 

25-Kuwalingania watu katika Uislamu kabla ya vita.

 

26-Ruhusa ya kupigana na waliolinganiwa Uislamu lakini wakakataa.

 

27-Kulingania kwa hekima kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((… na wajulishe wajibu wao katika haki ya Allaah)).

 

28-Kujua haki za Allaah (سبحانه وتعالى) katika Uislamu.

 

29-Thawabu za mtu kwa da’wah yake pindi akimwongoa mtu mwengine katika Uislamu.

 

30-Kuapa kwa jina la Allaah katika kuiunga mkono Fatwa ya Shariy’ah ya  Dini.

 

 

 

 

 

 

 

 

Share