16-Kitaab At-Tawhiyd: Mpaka Itakapoondolewa Fazaiko Nyoyoni Mwao, Watasema:

Mlango Wa 16

باب: حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ

Mpaka Itakapoondolewa Fazaiko Nyoyoni Mwao, Watasema: “Amesema Nini Rabb Wenu?”


 

 

قَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٢٣﴾

((Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao, watasema: “Amesema nini Rabb wenu?” Watasema: “Ya haki”; Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mkubwa wa dhati vitendo na sifa)) [Sabaa (34: 23)]

 

وفي الصحيح عن أبي هريرة  (رضي الله عنه) قال: قال رسول الله  (صلى الله عليه وسلم): ((إذَا قَضَى اللهُ الأَمْرَ فِي السَّمَاءِ ضَرَبَتِ الْمَلائِكَةُ بِأجْنِحَتِهَا خَضْعَاناً  لِقَوْلِهِ كَأَنَّهُ سِلْسِلَةٌ عَلى صَفْوَانٍ يَنْفُذُهُم ذَلِكَ: ((حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ)) فَيَسْمَعُهَا مُسْترَقُ السَّمْعِ .ومُسْترقُ السَّمْعِ هَكَذَا بَعْضُهُ فَوْقَ بَعْضٍ)). وَصَفَهُ سُفْيَانُ بِكِفِّهِ فَحَرَّفَهَا وبَدَّدَ بَيْنَ أصابِعِهِ: ((فَيَسْمَعُ الْكَلِمَةَ فَيُلقيها إلىَ مَنْ تَحْتَهُ، ثُمَّ يُلقِيهَا الآخَرُ إلىَ مَنْ تَحْتَهُ حتى َيُلقِيهَا عَلى لِسَانِ السَّاحِرِ أَوْ الْكَاهَنِ، فَرُبَّمِا أَدْرَكَهُ الشِّهابُ قَبْلَ أنْ يُلقِيهَا. وَرُبَّما ألْقاها قَبْلَ أَنْ يُدْرِكَهُ، فَيَكْذِبُ مَعَها مائةَ كَذْبَةٍ فَيُقالُ: أَلَيْسَ قَدْ قَال لنا يَوْمَ كَذا وَكَذا: كَذا وَكَذا فَيُصَدَّقُ بِتِلْكَ الْكَلِمَةِ الَّتِي سُمِعَتْ مِنَ السَّمَاءِ))

Na katika Swahiyh Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Allaah Anapohukumu jambo mbinguni, [na kumpa Wahyi Jibriyl],Malaika hupiga mbawa zao kwa kuinyenyekea kauli [ya wahyi wa Allaah], kwa vile Malaika husikia kama kwamba ni sauti za minyororo ya chuma inyoburutwa katika juu ya jiwe gumu. [Kauli hiyo ya Allaah] Huwakumba na kuwakhofisha hadi wazimie.  Hivyo, ((Mpaka itakapoondolewa khofu nyoyoni mwao; watasema: “Amesema nini Rabb wenu?” Watasema: “Ya haki”; Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mkubwa wa dhati vitendo na sifa)) Watasikia amri hii wasikivu wa siri [mashaytwaan].  Na wasikivu wa siri hao wako kama hivi; wanarundikana mmoja juu ya wengine)): Sufyaan alionyesha kwa kuunyanyua mkono wake na kutawanya vidole. ((Wadukizi [wezi wa maneno] husikia neno ambalo hulipeleka kwa aliyechini yake, na wa pili hulipeleka kwa aliye chini yake, hubadilishabadilisha katika kupokeana kauli hiyo mpaka wa mwisho wao ambaye hulipeleka kwa mchawi au kuhani. Mara nyingine kimondo humpiga shaytwaan kabla ya kuwahi kuipeleka [siri aliyosikia] na mara nyingine huwahi kuipeleka kabla kimondo hakijampiga. Hapo mchawi huongezea uongo wake mara mia kuhusu neno hilo. Watu [huku ulimwenguni] husema: Je [mchawi] hatukujulisha kadha na kadhaa siku kadhaa na kadhaa. Hivyo mchawi huaminiwa kwa kuwa kasema ukweli kutokana na kauli iliyosikika mbinguni)) [Al-Bukhaariy]

 

عن النَّوَّاس بن سمعان (رضي الله عنه)  قال:  قال رسول الله  (صلى الله عليه وسلم): ((إذا أرَادَ اللهُ تَعَالى أنْ يُوحِيَ بِالأمِرِ تَكلَّمَ بِالوَحْي أخذت السماوات منه رَجْفَةٌ أو قال رِعْدة شديدة، خوفاً من اللّه عز وجلّ، فإذا سَمعَ ذلك أهلُ السماوات صَعِقوا وخرُّوا لله سُجَّداً، فيكون أوَّل مَنْ يرفعُ رأسه جبريل، فيُكلِّمُهُ الله من وحيه بما أراد، ثم يَمُرُّ جبريل على الملائكة، كُلّماَ مرَّ بسماء سأله ملائكتُها: ماذا قال ربنا يا جبريل؟ فيقول جبريل : قال الحقَّ، وهو العلي الكبير، فيقولون كلّهم مِثل ما قال جبريل، فينْتهي جبريل بالوحي إلى حيثُ أمَرَهُ الله عز وجل))

Kutoka kwa An-Nawaas bin Sam’aan (رضي الله عنه)   amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Anapotaka kuleta Wahyi wa jambo, Hutamka na mbingu hutetemeka kwa nguvu)) Au kasema: ((Radi ya nguvu kwa kumkhofu Allaah ‘Azza wa Jalla. Wanapoyasikia Malaika wa mbinguni, huzimia au huporomoka na kusujudu. Wa kwanza anayeinua kichwa chake huwa ni Jibriyl. Kisha Allaah Humsemesha kumpa Wahyi Autakao. Kisha Jibriyl huwapitia Malaika. Kila anapopita mbingu moja Malaika humuuliza: Amesema nini Rabb wetu ee Jibriyl? Hujibu: [Amesema]: ((Ya haki”; Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mkubwa wa dhati vitendo na sifa)) Wote husema kama alivyosema Jibriyl. Jibriyl humalizia kuufikisha Wahyi alipoamrishwa na Allaah ‘Azza wa Jalla)) [Ibn Khuzaymah fiy At-Tawhiyd (206)]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Sabaa (34:23).

 

2-Yaliyomo humo miongoni mwa hoja kuu ya kubatilisha shirki hususani kwa wenye kutegemea waja wema kwa shafaa’ah. Aayahi hii inajulikana kuwa ndiyo inayokata mizizi ya shirki.

 

3-Tafsiri ya Aayah:

قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٢٣﴾

((Watasema: “Ya haki”; Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mkubwa wa dhati vitendo na sifa))

  

4- Sababu ya wao (Malaika) kuuliza swali hilo (katika Aayah)

 

5-Baada ya hapo, Jibriyl alijibu swali lao kwa kusema, “Amesema kadhaa wa kadhaa.”

 

6-Kutajwa kuwa wa kwanza atakayeinua kichwa chake ni Jibriyl.

 

7-Jibriyl huwaambia wote Malaika wote walioko mbinguni kwa sababu wamemuuliza.

 

8-Athari ya tetemeko linawaenea wakazi wote wa mbinguni.

 

9-Jinsi mbingu zinavyotetemshwa kutokana na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى).

 

10-Jibriyl ndiye anayepeleka Wahyi mahali Anapomwamuru Allaah (سبحانه وتعالى).

 

11-Kuhusu udukuzi wa shaytwaan (kusikiliza siri).

 

12-Kupandiana kwa majini mmoja juu ya mwingine.

 

13-Kufyatuliwa vimondo vya moto.

 

14-Wakati mwingine vimondo vinamwangamiza shaytwaan kabla hawajafikisha khabari, na wakati mwingine humwangamiza baada ya kuifikisha khabari katika sikio la rafiki yake; shaytwaan bin Aadam.

 

15-Wakati mwingine kuhani (au mtabiri) huenda akasema ukweli.

 

16-Pamoja na ukweli huo huongezea uongo mara mia. 

 

17-Utabiri wa watabiri huenda mara nyingine ukawa ni ukweli, lakini hayo hutegemea na yaliyosikika mbinguni. 

 

18-Watu kukubali uongo (wa mtabiri). Wanawezaje kutegemea ukweli mmoja na kutokuzingatia mara 99 ya uongo wake?

 

19-Jinsi wanavyopashana maneno na wanayahifadhi na kuyatumia dalili (ya uongo mwingine).

 

20-Uthibitisho wa Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) kinyume na madai ya Ash‘ariyyah[1] na Mu’attwilah.

 

21-Ngurumo na tetemeko la mbingu ni kwa ajili ya kumkhofu Allaah (سبحانه وتعالى).

 

22-Malaika wanaporomoka chini kumsujudia Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya kusikia maneno Yake.

 

 

 

[1] Watu wanaojinasibisha kwa ‘Abul-Hasan Ash´ariyy ambao wanakanusha Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) Alizozithibitisha katika Qur-aan kuhusu mikono, miguu n.k. Lakini alitubia na akarudia katika msimamo wa Ahlus-Sunnah. 

 

 

Share