62-Kitaab At-Tawhiyd: Makatazo Ya Kuapa Kwa Wingi

Mlango Wa 62

بَابٌ مَا جَاءَ فِي كَثْرَةِ الْحَلِفِ

Makatazo Ya Kuapa Kwa Wingi


 

 

وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ

((Na hifadhini yamini zenu)) [Al-Maaidah (5: 89)]

  

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  يَقُولُ:  ((الْحَلِفُ مَنْفَقَةٌ لِلسِّلْعَةِ مَمْحَقَةٌ لِلْكَسْبِ)) أَخْرَجَاهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه)  amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Kwa kuapa, [muuzaji] huenda akamshawishi  mnunuaji kununua bidhaa, lakini kunafuta Baraka za Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

وَعَنْ سَلْمَانَ: أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((ثَلاثَةٌ لاَ يُكَلِّمُهُمْ اَللَّهُ وَلاَ يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ: أُشَيمِطٌ زَانٍ وَعَائِلٌ مُسْتَكْبِرٌ وَرَجُلٌ جَعَلَ اَللَّهَ بِضَاعَتَهُ لاَ يَشْتَرِي إِلاَّ بِيَمِينِهِ وَلاَ يَبِيعُ إِلاَّ بِيَمِينِه)) رَوَاهُ اَلطَّبَرَانِيُّ بِسَنَدٍ صَحِيحٍ

Na Imepokelewa kutoka kwa Salmaan kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Watu watatu ambao Allaah Hatowasemesha, wala Hatowatakasa, na watapata adhabu kali: Mzinifu mzee, maskini anayetakabari, na mtu aliyejaaliwa na bidhaa, lakini hanunui ila kwa kuapa [wa-Allaahi] na hauzi ila kwa kuapa [wa-Allaahi)) [At-Twabaraaniy kwa isnaad Swahiyh]

 

وَفِي اَلصَّحِيحِ: عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَينٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((خَيْرُ أُمَّتِي قَرْنِي، ثُمَّ اَلَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ اَلَّذِينَ يَلُونَهُمْ)) قَالَ عِمْرَانُ:  فَلا أَدْرِي أَذَكَرَ بَعْدَ قَرْنِهِ مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلاثًا؟ ((ثُمَّ إِنَّ بَعْدَكُمْ قَوْمًا يَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْهَدُونَ، وَيَخُونُونَ وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ، وَيَنْذِرُونَ وَلاَ يُوفُونَ، وَيَظْهَرُ فِيهِمْ اَلسِّمَن))   

Na katika Swahiyh (Muslim) kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ummah bora kabisa ni karne yangu, kisha wale wanaowafuatia, kisha wanowafuatia)) ‘Imraan akasema: “Lakini sijui kama alitaja mara mbili baada ya karne yake au tatu?.” ((Kisha watakuja watu baada yenu, kushuhudia bila ya kuombwa kutoa ushahidi, na watakuwa makhaini wala hawatoaminiwa, na wataweka nadhiri lakini hawatotimiza, na itadhihirika kwao unene))[1]

 

وَفِيهِ عَنِ اِبْنِ مَسْعُود: ٍ أَنَّ اَلنَّبِيَّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((خَيْرُ اَلنَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ اَلَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ اَلَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ يَجِيءُ قَوْمٌ تَسْبِقُ شَهَادَةُ أَحَدِهِمْ يَمِينَهُ وَيَمِينُهُ شَهَادَتَهُ))

Na humo (katika Muslim) imesimuliwa kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wale wanaowafuatia, kisha wanowafuatia, kisha watakuja watu ambao ushahidi wao utatangulia viapo vyao na viapo vitatangulia ushahidi wao))[2]

 

قَالَ إِبْرَاهِيمُ كَانُوا يَضْرِبُونَنَا عَلَى اَلشَّهَادَةِ وَالْعَهْدِ وَنَحْنُ صِغَارٌ 

Ibraahiym (An-Nakha’iyy) amesema: “Tulikuwa tukichapwa (na wazee wetu) tulipokuwa wadogo juu ya jambo la kuapa na kutoa ushahidi.”

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Wasia juu ya kulinda viapo.

 

2-Tanbihi kuwa japokuwa viapo vinasaidia uuzaji wa bidhaa lakini hakuna baraka katika pato la mtu.

 

3-Tishio la adhabu kali kwa wale ambao hawanunui au kuuza isipokuwa kwa kiapo.

 

4-Onyo kuwa kutenda dhambi kwa sababu ndogondogo au pasina sababu hukuza ukubwa wa dhambi.

 

5-Karipio kwa wanaoapa pasi na kutakiwa kufanya hivyo.

 

6-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kusifu vizazi vitatu au vine vya kwanza na maelezo ya kitakachotokea baadaye.

 

7-Watatoa ushahidi pasina kutakiwa hivyo.

 

8-As-Salaf walikuwa wakiwachapa watoto wao kwa kuapa au kutoa ushahidi ovyo.

 

 

 

 

 

[1] Kutokana na kughafilishwa na mambo ya dunia.

[2] Kwa sababu hawatolipa uzito jukumu lao la kutoa ushahidi na kula viapo kwa hivyo watakuwa wepesi wa kutoa ushahidi na kula viapo bila ya kujaili.

Share