67-Kitaab At-Tawhiyd: Hawakumthamini Allaah Ipasavyo Kumthamini

Mlango Wa 67

باب:  وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ

Hawakumthamini Allaah Ipasavyo Kumthamini


 

  قَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٧﴾

((Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itakamtwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa! Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha)) [Az-Zumar (39: 67)]

 

عَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: جَاءَ حَبْرٌ مِنَ الأَحْبَارِ إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ! إِنَّا نَجِدُ أَنَّ اَللَّهَ يَجْعَلُ اَلسَّمَاوَاتِ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالأَرَضِينَ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالشَّجَرَ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالْمَاءَ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالثَّرَى عَلَى إِصْبَعٍ، وَسَائِرَ الْخَلْقِ عَلَى إِصْبَعٍ، فَيَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ. فَضَحِكَ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حَتَّى بَدَتْ نَوَاجِذُهُ، تَصْدِيقًا لِقَوْلِ الْحَبْرِ، ثُمَّ قَرَأَ: (( وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ))

Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه)  amesema: Alikuja mwanachuoni wa Kiyahudi  kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Muhammad! Tumejua kwamba Allaah Ataziweka mbingu zote katika kidole kimoja, na ardhi zote katika kidole kimoja, na miti katika kidole kimoja, na maji na vumbi katika kidole kimoja, na viumbe vyote vinginevyo katika kidole kimoja. Kisha Atasema: Mimi Ndiye Mfalme.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akacheka mpaka meno yake ya magego yakaonekana kwa kukubali maneno ya Myahudi, kisha (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم akasoma Aayah: ((Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itakamtwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah)) 

 

وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: ((وَالْجِبَالَ وَالشَّجَرَ عَلَى إِصْبَعٍ، ثُمَّ يَهُزُّهُنَّ فَيَقُولُ: أَنَا الْمَلِكُ أَنَا اَللَّهُ!))

Na katika riwaayah ya Muslim: ((Na milima na miti katika kidole kimoja, kisha Ataitingisha na Aseme: Mimi Ndiye Mfalme, Mimi Ndiye Allaah!))

 

وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ: ((وَيَجْعَلُ اَلسَّمَاوَاتِ عَلَى إِصْبَعٍ وَالْمَاءَ وَالثَّرَى عَلَى إِصْبَعٍ، وَسَائِرَ الْخَلْقِ عَلَى إِصْبَعٍ)) . أَخْرِجَاهُ

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: ((Na Ataweka mbingu katika kidole kimoja, na maji na mchanga katika kidole kimoja, na viumbe vyote vilobakia katika kidole kimoja)) 

 

وَلِمُسْلِمٍ عَنْ اِبْنِ عُمَرَ مَرْفُوعًا: ((يَطْوِي اَللَّهُ اَلسَّمَاوَاتِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ثُمَّ يَأْخُذُهُنَّ بِيَدِهِ الْيُمْنَى، ثُمَّ يَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ أَيْنَ الْجَبَّارُونَ؟ أَيْنَ الْمُتَكَبِّرُونَ؟ ثُمَّ يَطْوِي الأَرْضِينَ اَلسَّبْعَ، ثُمَّ يَأْخُذُهُنَّ بِشِمَالِهِ، ثُمَّ يَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ، أَيْنَ الْجَبَّارُونَ؟ أَيْنَ الْمُتَكَبِّرُونَ؟))

Na Muslim amesimulia kutoka kwa Ibn ‘Umar Hadiyth Marfuw’: ((Allaah Atakunja mbingu Siku ya Qiyaamah kisha Atazichukua katika Mkono Wake wa kuume kisha Atasema: Mimi Ndiye Mfalme, wako wapi majabari? Wako wapi [leo] wanaotakabari? Kisha Atakunja ardhi saba kisha Atazichukua katika Mkono Wake wa kushoto kisha Atasema: Mimi Ndiye Mfalme, wako wapi majabari, wako wapi [leo] wanaotakabari?))

 

وَرُوِيَ عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: مَا اَلسَّمَاوَاتُ اَلسَّبْعُ وَالْأَرْضُونَ اَلسَّبْعُ فِي كَفِّ اَلرَّحْمَنِ إِلَّا كَخَرْدَلَةٍ فِي يَدِ أَحَدِكُمْ  

Na imesimuliwa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kasema: “Mbingu saba na ardhi saba si chochote ila kama kama chembe ya hardali katika mkono wa mmoja wenu.”

 

وَقَالَ اِبْنُ جَرِيرٍ: حَدَّثَنِي يُونُسُ، أَخْبَرَنَا اِبْنُ وَهْبٍ، قَالَ: قَالَ اِبْنُ زَيْدٍ: حَدَّثَنِي أَبِي، قَالَ :قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَا اَلسَّمَاوَاتُ اَلسَّبْعُ فِي الْكُرْسِيِّ إِلاَّ كَدَرَاهِمَ سَبْعَةٍ أُلْقِيَتْ فِي تُرْسٍ))  قَالَ: وَقَالَ أَبُو ذَرٍّ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ يَقُول:ُ ((مَا الْكُرْسِيُّ فِي الْعَرْشِ إلاَّ كَحَلْقَةٍ مِنْ حَدِيدٍ أُلْقِيَتْ بَيْنَ ظَهْرَيْ فَلاةٍ مِنَ الأَرْضِ))

Na Ibn Jariyr amesema: “Yuwnus amenihadithia: Tulijulishwa na Ibn Wahb amesema: Ibn Zayd amesema: Baba yangu amenihadithia, akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mbingu saba kulingana na Al-Kursiy ya Allaah, ni ndogo mno kama dirham saba zilowekwa katika ngao ya askari)) Akasema Abuu Dharr: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Al-Kursiy kulingana na ‘Arshi ni kama kikuku cha chuma kilotupwa baina ya uwanja mkubwa))

 

Al-Kursiy: Kiti cha Enzi kinachomhusu Allaah Pekee.  

 

وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ  قَالَ: ((بَيْنَ اَلسَّمَاءِ اَلدُّنْيَا وَاَلَّتِي تَلِيهَا خَمْسُمِائَةِ عَامٍ،  وَبَيْنَ كُلِّ سَمَاءٍ وَسَمَاءٍ خَمْسُمِائَةِ عَامٍ، وَبَيْنَ اَلسَّمَاءِ اَلسَّابِعَةِ وَالْكُرْسِيِّ خَمْسُمِائَةِ عَامٍ، وَبَيْنَ الْكُرْسِيِّ وَالْمَاءِ خَمْسُمِائَةِ عَامٍ، وَالْعَرْشُ فَوْقَ الْمَاءِ، وَاَللَّهُ فَوْقَ الْعَرْشِ، لاَ يَخْفَى عَلَيْهِ شَيْءٌ مِنْ أَعْمَالِكُمْ)).  أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَهْدِيٍّ عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ عَنْ عَاصِمٍ عَنْ زِرٍّ عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ. 

وَرَوَاهُ بِنَحْوِهِ الْمَسْعُودِيُّ عَنْ عَاصِمٍ عَنْ أَبِي وَائِلٍ عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ. قَالَهُ الْحَافِظُ اَلذَّهَبِيُّ رَحِمَهُ اَللَّهُ، قَالَ:وَلَهُ طُرُقٌ

Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه)  amesema: ((Masafa ya baina ya mbingu ya kwanza na dunia  ni mwendo wa miaka mia tano, na baina ya kila mbingu na nyingine miaka mia tano. Na baina ya mbingu saba na Al-Kursiyy pia ni miaka mia tano. Na   baina ya Al-Kursiyy na maji ni miaka mia tano. ‘Arshi (ya Allaah) iko juu ya maji na Allaah Yuko juu ya ‘Arshi, hakifichiki chochote katika vitendo vyenu.” [Imeripotiwa na Ibn Mahdi kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa ‘Aaswim kutoka kwa Zirr, kutoka kwa ‘Abdullaah (Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه) ]

 

Na imesimuliwa na Al-Haafhidwh Adh-Dhahabiyy amesema: “Hadiyth hiyo ina njia nyingi.”

 

وَعَنْ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((هَلْ تَدْرُونَ كَمْ بَيْنَ اَلسَّمَاءِ وَالأَرْضِ؟)) قُلْنَا: اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: ((بَيْنَهُمَا مَسِيرَةُ خَمْسُمِائَةِ سَنَةٍ، وَمِنْ كُلِّ سَمَاءٍ إِلَى سَمَاءٍ، مَسِيرَةُ خَمْسُمِائَةِ سَنَةٍ، وَكِثَفُ كُلِّ سَمَاءٍ مَسِيرَةُ خَمْسِمِائَةِ سَنَةٍ، وَبَيْنَ اَلسَّمَاءِ اَلسَّابِعَةِ وَالْعَرْشِ بَحْرٌ بَيْنَ أَسْفَلِهِ وَأَعْلاهُ كَمَا بَيْنَ اَلسَّمَاءِ وَالأَرْضِ، وَاَللَّهُ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى فَوْقَ ذَلِكَ، وَلَيْسَ يَخْفَى عَلَيْهِ شَيْءٌ مِنْ أَعْمَالِ بَنِي آدَمَ))  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَغَيْرُهُ

Na Imepokelewa toka kwa Al-’Abbaas bin ‘Abdil-Muttwalib(رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Je, mnajua masafa mangapi yapo baina ya mbingu na ardhi?)) Tukasema: “Allaah na Rasuli Wake wanajua.”  Akasema: ((Masafa baina yake ni mwendo wa miaka mia tano, na masafa baina ya mbingu moja na ya pili yake inayofuatia ni mwendo wa miaka mia tano. Na unene wa kila mbingu ni sawa na mwendo wa miaka mia tano. Na baina ya mbingu ya saba na ‘Arshi kuna bahari; kina chake ni sawa na umbali wa baina mbingu na ardhi. Na Allaah Yuko juu ya hivyo hakifichiki chochote katika vitendo vya bin Aadam)) [Abuu Daawuwd na wengineo]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Tafsiri ya Aayah Suwrah Az-Zumar (39: 67).

وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

((Na hali ardhi yote itakamtwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah)).

 

2-Elimu ya mambo haya yalikuwepo kwa Wayahudi wakati wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na hawakulikanusha wala kulieleza.

 

3-Pale Rabai wa dini ya Kiyahudi alipomtajia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mambo hayo, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alithibitisha kauli yake na Wahyi wa Qur-aan uliteremka kuthibitsha hilo (alilolitaja).

 

4-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kucheka katika kuthibitisha elimu kubwa aliyoyasema Rabai wa dini ya Kiyahudi. 

 

5-Kutajwa Mikono miwili ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba mbingu zitakuwa katika Mkono Wake wa kuume na ardhi katika Mkono Wake wa kushoto.   

 

6- Mkono wa pili uliitwa wa kushoto.

 

7-Pamoja na hayo kumetajwa majabari na wenye kutakabari.

 

8-Kauli kwamba mbingu saba na ardhi katika Mkono wa Allaah (سبحانه وتعالى) zitakuwa kama chembe ya hardali mikononi wa mmoja wenu.

 

9-Ukubwa wa Al-Kursiyy (Kiti cha enzi cha Allaah سبحانه وتعالى) kulingana na mbingu.

 

10-Ukubwa wa Al-‘Arsh kulingana na Al-Kursiyy.

 

11-Kwamba Al-Kursiyyi, maji, na Al-‘Arsh ni vitu tofauti.

 

12-Umbali baina ya mbingu moja na nyingine.

 

13-Umbali baina mbingu ya saba na Al-Kursiyy.

 

14-Umbali baina ya Al-Kursiyy na maji.

 

15-‘Arshi ya Allaah (سبحانه وتعالى) iko juu ya maji.

 

16-Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu ya Al-‘Arsh.

 

17-Umbali baina ya mbingu na ardhi.

 

18-Unene wa kila mbingu ni masafa ya mwendo wa miaka mia tano.

 

19- Bahari juu ya mbingu ya saba ina kina cha masafa ya mwendo wa miaka mia tano. Na Allaah Anajua zaidi

 

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah (سبحانه وتعالى) Rabb wa walimwengu. Swalaah na Salaam zimshukie Nabiyyunaa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba wake wote (رضي الله عنهم).

 

 

 

Share