008-Aayah Na Mafunzo: Alama Za Unafiki

Aayah Na Mafunzo:

Al-Baqarah

Alama Za Unafiki

 

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ 

8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini.

 

Mafunzo:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((آيَةُ الْمُنَافِقِ ثلاَثٌ إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ)) متفق عليه . وفي رواية: ((وَإِنْ صَامَ وَصَلَّى وَزَعَمَ أَنَّهُ مُسْلِمٌ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Alama za mnafiki ni tatu: anapozungumza husema uongo, anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi), na anapoaminiwa hufanya khiyana)) [Al-Bukhaariy, Muslim] Na katika riwaaya nyingine: ((Hata akifunga na akiswali na akidai kuwa yeye ni Muislamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

 

Share