023-Aayah Na Mafunzo: Changamoto Hawezi Yeyote Kuleta Mfano wa Qur-aan

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Changamoto Hawezi Yeyote Kuleta Mfano wa Qur-aan

 

 

 

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾

24. Msipofanya, na wala hamtoweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri.

 

Mafunzo:

 

Changamoto kama hiyo Anasema Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa)

 

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٣﴾

13. Je, wanasema ameitunga (hii Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasina Allaah mkiwa ni wakweli.  [Huwd: 13]

 

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾

88. Sema: “Ikiwa watajumuika wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.”  [Al-Israa: 88]

 

 

Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Na hii ni dalili ya kikomo na burhani ya wazi kuthibitisha aliyokuja nayo Rasuli na akayasadikisha pindi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anapowapa changamoto ya kuwapinza wana Aadam na majini walete Qur-aan mfano wake, Akawajulisha kwamba hawawezi kuleta mfano wake hata kama watashirikiana wote kufanya hivyo basi hawataweza kamwe!”.

 

 

 

 

 

Share