034-Aayah Na Mafunzo: Maasi Ya Kwanza Ni Kibri. Hatoingia Jannah Mwenye Chembe Ya Kibri

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Maasi Ya Kwanza Ni Kibri. Hatoingia Jannah Mwenye Chembe Ya Kibri

 

 

 

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na pale Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.

 

Mafunzo:

 

Qataadah alisema kuhusu kauli ya Allaah: Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.” “Ibliys ni adui wa Allaah. Alimwonea wivu Aadam kwa sababu Allaah Alimtukuza Aadam. Alisema (Ibliys). “Nimeumbwa kwa moto naye (Aadam) kaumbwa kwa udongo!” Kwa hiyo kosa la kwanza kufanywa lilikuwa ni kibri, kwani adui wa Allaah alikuwa na kibri sana kumsujudia Aadam.” Mimi (Ibn Kathiyr) nasema: yameandikwa katika Swahiyh: “Hakuna atakayeingia Jannah mtu ambaye ana kiburi chenye uzito sawa na punje ya khardali.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share