219-Aayah Na Mafunzo: Kafara Ya Niyyah Ya Kucheza Kamari Ni Kutoa Swadaqah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kafara Ya Niyyah Ya Kucheza Kamari Ni Kutoa Swadaqah

 

 

 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

219. Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na  shariy’ah) ili mpate kutafakariMafunzo:

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuapa akasema katika kiapo chake: Naapa kwa Laata na ‘Uzzaa (majina ya waabudiwa wa uongo) aseme: Laa ilaaha illa Allaah. Na atakayemwambia mwenzake: Njoo tuchezeshe kamari, basi atoe swadaqah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share