257-Aayah Na Mafunzo: Du’aa Ya Kuomba Kutolewa Kizani Na Kuingia Katika Nuru

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Du’aa Ya Kuomba Kutolewa Kizani Na Kuingia Katika Nuru

 

www.alhidaaya.com

 

 

 اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾

257. Allaah ni Mlinzi Msaidizi wa wale walioamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika Nuru. Na wale waliokufuru marafiki wao wandani ni twaghuti, huwatoa kutoka katika Nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa motoni wao humo ni wenye kudumu.

 

Mafunzo:

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) alikuwa akitufundisha maneno mengine lakini hakuyafundisha kama alivyokuwa akitufundisha tashahhud: 

 

((اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا وَأَبْصَارِنَا وَقُلُوبِنَا وَأَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا))

Allaahumma allif bayna quluwbinaa, wa Aswlih dhaata bayninaa, wahdinaa subulas-ssalaami, wanajjinaa minadhw-dhwulumaati ilan-nnuwri, wa jannibnal-fawaahisha maa dhwahara minhaa wamaa batwan, wa Baarik-lanaa fiy asmaa’inaa, wa abswaarinaa, wa quluwbinaa, wa azwaajinaa, wa dhurriyaatinaa, watub ‘alaynaa Innaka Antat-Tawaabur-Rahiym, waj-’alnaa shaakiriyna lini’matika muthniyna bihaa qaabiliyhaa wa atimmahaa ‘alaynaa

 

Ee Allaah, unganisha baina ya nyoyo zetu, na Suluhisha yaliyo baina yetu na Tuongoze njia ya amani, na Tuokoe kutokana na kiza na kutuingiza katika Nuru, na Tuepushe machafu ya dhahiri na ya siri, na Tubarikie katika kusikia kwetu na kuona kwetu, nyoyo zetu, na wake zetu, na vizazi vyetu, na Tupokelee tawbah zetu, hakika Wewe ni At-Tawwaabur-Rahiym  (Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye Kurehemu) na Tujaalie kuwa wenye kushukuru neema Zako, mwenye kukusifu kwazo wakati wa kuzipokea na zitimize kwetu. [Abuu Daawuwd, Al-Haakim akasema ‘Swahiyh kwa sharti ya Muslim, na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/265) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad (490)].

 

 

Share