264-Aayah Na Mafunzo: Mfano Anayetoa Swadaqah Kwa Riyaa Kuwa Hapati Thawabu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Mfano Anayetoa Swadaqah Kwa Riyaa (Kujionyesha) Kuwa Hapati Thawabu

 

 Alhidaaya.com

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

264. Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.

 

 

Mafunzo:

 

عنْ ابي هريرة رضي الله عنه أنَّه صلَّى الله عليه وسلَّم قال: ((قال الله تعالى: أنا أغْنى الشُّركاء عن الشِّرْك، فمَن عمل عملاً أشْرَك فيه معي غيري تركتُه وشِرْكه))    

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Ta’aalaa Anasema: Mimi Ni Mwenye kujitosheleza kabisa, Sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye amali kwa kunishirikisha na mtu, Nitaikanusha pamoja na mshirika wake.”  Yaani: hatopata ujira wowote kwa amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)]

 

 

Share